Vijana Na Michezo
Timu ya kitaifa ya Misri yaweka tarehe ya mechi ya Malawi katika uwanja wa Kairo katika Fainali za kufikia Mataifa ya Afrika
Nour Khalid
Machi 24 ijayo imeandaliwa kuwa tarehe ya mechi ya timu ya kitaifa ya Misri na timu ya kitaifa ya Malawi katika uwanja wa kimataifa wa Kairo katika raundi ya tatu kwa Fainali za kufikia Kombe la Mataifa ya Afrika, itakayofanyika huko Côte d’lvoire mnamo Januari 2024.
Mchezo wa timu ya kitaifa ya Misri dhidi ya Malawi umepangwa kufanyika saa tatu usiku, kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo
Wakati timu ya kitaifa ya Malawi ilipanga tarehe Machi 28, mnamo saa tisa mchana kuwa mwenyeji wa timu ya kitaifa ya Misri katika raundi ya nne ya Fainali za Mataifa ya Afrika.