Vijana Na Michezo

Ushindi wa Congo na Uganda katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana

Nour Khalid

 

Timu ya kitaifa ya Congo imeshinda mwenzake wa Sudan Kusini kwa 2/1, pia timu ya kitaifa ya Uganda imeshinda timu ya kitaifa ya Afrika ya Kati kwa 2/1 katika raundi ya kwanza kutoka mechi za kundi la pili la kombe la Mataifa ya Afrika, zinazofanyika nchini Misri kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20.

Katika mechi ya kwanza timu ya kitaifa ya Congo ilipiga goli katika dakika ya 45, kisha Prans Aldi Sosoyo akipiga goli la pili katika dakika ya 63 lakini Paul Amerka Gawa alipiga goli la kwanza na la mwisho kutoka timu ya kitaifa ya Sudan Kusini katika dakika la 83.

Katika mechi nyingine, Isma Mogolosi na John Paul Dembe waliifungia Uganda mabao katika dakika ya 47 na 74, na Boris Gbeno aliihakikishia Afrika ya Kati bao pekee katika sekunde za mwisho za mchezo huo. Congo na Uganda ziliongoza Kundi B zikiwa na pointi tatu kwa kila moja .

Back to top button