Habari
MAMA MARIAM MWINYI APONGEZWA NA UVCCM ,UVCCM KUJIPANGA NA MATEMBEZI YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MWAKANI
Ahmed Hassan
Mlezi wa Matembezi ya UVCCM ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mke wa Rais Zanzibar ,Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Rehema Omary Sombi na ujumbe wake waliofika Ofisi za ZMBF, Ikulu Migombani.
Naye ,Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Sombi amempongeza Mama Mariam Mwinyi kwa kutimiza Mwaka mmoja wa Taasisi yake ya ZMBF, pia kwa mafanikio ya kazi nzuri kwa kuwawezesha Wanawake wakulima wa mwani,kupambana na vitendo vya udhalilishaji kwa watoto na kuwa kinara wa hamasa katika kushiriki kuhamasisha ufanyaji wa Mazoezi katika matembezi ya Kila mwisho wa Mwezi kwa mapambano ya Magonjwa yasiyoambukiza.
Aidha, Mama Mwinyi amewataka UVCCM kuwa Mabalozi wa kitaifa kwa kuwasemea , kukemea Vitendo vya udhalilishaji kwa Watoto kuibeba kama ajenda ya Kitaifa wanapozunguka Mikoa ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.
Pia amewapongeza UVCCM kwa Kusukuma gurudumu la maendeleo la Jumuiya yao na Taifa kwa ujumla.
Mama Mwinyi amewataka kuwa ubunifu zaidi Katika shamrashamra za matembezi ya kuadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwakani kwa kuja na mbinu tofauti kwa kuibua miradi ya vijana kwa maendeleo na kuendelea kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .