Habari Tofauti

Spika wa Bunge la Zimbabwe atembelea Mkoa wa Aswan

Ali Mahmoud

Mheshimiwa Jacob Mudenda, Spika wa Bunge la Zimbabwe, alitembelea Mkoa wa Aswan katika mfumo wa ziara yake rasmi nchini Misri kwa mwaliko kutoka kwa Mshauri Dkt. Hanafi Jebali, Spika wa Bunge, kujadili njia za kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili, haswa katika ngazi ya bunge, na katika mfumo wa nia ya Misri kuendeleza mahusiano na ndugu Barani Afrika.

Wakati wa ziara ambayo alisindikizwa na Katibu Mkuu wa Mkoa wa Aswan na maafisa kadhaa wakuu katika Mkoa huo, Spika wa Bunge la Zimbabwe alikagua vivutio vya utalii katika Mkoa huo na kufahamu kwa ukaribu, historia ya ustaarabu wa Misri.

Pia alitembelea jengo la Benban la Nishati ya Jua mkoani Aswan kama mfano wa vituo vya hali ya juu vya Nishati ya Jua.

Back to top button