Rais El-Sisi apokea ujumbe wa wakuu wa mabaraza na mabunge ya kiarabu na wakuu wa wajumbe wanaoshiriki mkutano wa tano wa Bunge la Kiarabu
Ali Mahmoud

Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi alipokea ujumbe wa wakuu wa mabaraza na mabunge ya kiarabu na wakuu wa wajumbe wanaoshiriki katika mkutano wa tano wa Bunge la Kiarabu, kwa mahudhurio ya Mheshimiwa Adel Al-Assoumi, Mwenyekiti wa Bunge la Kiarabu, na Mheshimiwa “Chef Charumbira”, Spika wa Bunge la Afrika, mgeni wa heshima wa mkutano huo, na kwa upande wa Misri, Dkt. Hanafi Jebali, Mwenyekiti wa Bunge.
Katika taarifa ya Mshauri Ahmed Fahmy, Mzungumzaji rasmi wa Urais wa Jamhuri, alisema kuwa Mheshimiwa Rais aliwakaribisha Wakuu wa mabunge ya Kiarabu, mwanzoni mwa mkutano huo, akisisitiza msaada wa Misri kwa juhudi za kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa bunge kati ya nchi za kiarabu kwa njia ambayo inachangia kubadilishana uzoefu na kuendeleza mchakato wa ushirikiano kati ya nchi za kiarabu. Pia, Mheshimiwa Rais alitathmini uamuzi wa Bunge la Kiarabu, wakati wa kikao cha sasa cha mkutano, kwa kuzingatia juu ya mada ya usalama wa chakula, ambayo muhimu wake unazidi kutokana na mgogoro wa chakula ulimwenguni ambao ulimwengu unapitia.
Kwa upande wao, waheshimiwa waliohudhuria walisisitiza uangalifu wa mkutano wa Bunge la kiarabu wa kuendeleza dira ya pamoja ya bunge kuchangia kuimarisha kazi ya kiarabu na kukabiliana na changamoto zinazolikabili taifa hilo la kiarabu. Pia walitathmini juhudi za Misri kwa uongozi wa Mheshimiwa Rais na misimamo yake ya heshima na zinazosifiwa katika kulinda usalama wa kitaifa wa kiarabu, wakionesha shukrani za watu wa nchi za kiarabu kwa njia ya kisiasa na kimaendeleo ambayo Misri imefuata katika miaka iliyopita, iliyowezesha kuhimili changamoto kubwa ambazo zimeathiri eneo hilo. Katika muktadha huo, Mheshimiwa Rais alisisitiza umuhimu wa kudumisha mshikamano kati ya nchi za Kiarabu, akielezea nia ya Misri kuimarisha mahusiano ya Pamoja ya Kiarabu na kuziunga mkono nchi zote za kiarabu katika juhudi zao za kufikia utulivu na maendeleo, akisisitiza kuwa utulivu na amani ya kila nchi ya kiarabu ni utulivu na amani kwa Misri.