Habari Tofauti

Mkutano na Maonesho ya Matengenezo ya Ndege Barani Afrika na Mashariki ya Kati yazinduliwe

Mervet Sakr

Luteni Jenerali Mohamed Abbas, Waziri wa Usafiri wa Anga wa Misri, alizindua Mkutano na Maonesho ya Matengenezo na Mafunzo ya Ndege Barani Afrika na Mashariki ya Kati katika toleo lake la 31, kwa ushiriki wa wataalamu 400 wa masuala ya anga ya Shirika la ndege la Misri kwa ajili ya matengenezo na kazi za kiufundi.


Mkutano huo unaangaliwa sana kwa mashirika ya ndege ya kimataifa na ya Afrika na mamlaka husika, kwani ni jukwaa linalowaleta pamoja chini ya paa moja watoa huduma wengi wa matengenezo ya ndege, marekebisho na mafunzo, na hutoa fursa ya kufanya mikutano madhubuti baina ya washiriki kujadili masuala ya ushirikiano.

Vikao vya mkutano huo pia vinashuhudia majadiliano ya jopo la mada mbalimbali kwa kushirikisha wataalamu wakuu wa usafiri wa anga katika kanda hiyo, yanayolenga kubadilishana uzoefu na kupendekeza ufumbuzi wa ubunifu wa kuendeleza sekta ya usafiri wa anga kwa ujumla na matengenezo ya ndege na mafunzo haswa.

Maonesho hayo yanajumuisha makampuni makubwa yanayofanya kazi katika uwanja wa matengenezo ya ndege na marekebisho Barani Afrika na Mashariki ya Kati, mbali na watengenezaji wa ndege, injini na sehemu, wauzaji wa vipuri na kampuni za teknolojia ya usafiri wa anga kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambayo ni fursa ya masoko ya kuahidi kwa shughuli mbalimbali za matengenezo ya ndege na utoaji wa huduma mbalimbali za kiufundi na huduma mbalimbali za mafunzo, kwani idadi ya washiriki katika maadhimisho hayo inatarajiwa kuzidi wataalamu na wafanyakazi 400 wa usafiri wa anga katika fani hiyo.

 

Back to top button