Shirika la ndege la Misri yakaribisha Mkutano wa Kimataifa wa Matengenezo ya Ndege Barani Afrika na Mashariki ya Kati
Mervet Sakr

Shirika la ndege la Misri, inayowakilishwa na Kampuni ya Matengenezo na Kazi za Ufundi, itakuwa mwenyeji wa Mkutano na Maonesho ya Matengenezo na Mafunzo ya Ndege Barani Afrika na Mashariki ya Kati katika toleo lake la 31 katika kipindi cha kuanzia tarehe 5-7 Februari, ndani ya mfumo wa maagizo ya uongozi wa kisiasa wa kuendeleza sekta ya usafiri wa anga, na kuimarisha ushirikiano na ndugu wa Kiafrika katika shughuli mbalimbali za usafiri wa anga na chini ya uangalizi wa Wizara ya Usafiri wa Anga.
Mkutano huo unaangaliwa sana kwa mashirika ya ndege ya kimataifa na ya Afrika na mamlaka husika, kwani ni jukwaa linalowaleta pamoja chini ya paa moja watoa huduma wengi wa matengenezo ya ndege, marekebisho na mafunzo, na hutoa fursa ya kufanya mikutano madhubuti baina ya washiriki kujadili masuala ya ushirikiano, na vikao vya mkutano pia vinashuhudia majadiliano ya jopo la mada mbalimbali kwa kushirikisha wataalamu mashuhuri wa usafiri wa anga katika kanda na lengo la kubadilishana uzoefu na kupendekeza ufumbuzi wa ubunifu wa kuendeleza sekta ya usafiri wa anga kwa ujumla na matengenezo ya ndege na mafunzo haswa.
Maonesho hayo yanajumuisha makampuni makubwa yanayofanya kazi katika uwanja wa matengenezo ya ndege na marekebisho Barani Afrika na Mashariki ya Kati, mbali na watengenezaji wa ndege, injini na sehemu, wauzaji wa vipuri na kampuni za teknolojia ya usafiri wa anga kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambayo ni fursa ya masoko ya kuahidi kwa shughuli mbalimbali za matengenezo ya ndege na utoaji wa huduma mbalimbali za kiufundi na huduma mbalimbali za mafunzo, kwani idadi ya washiriki katika maadhimisho hayo inatarajiwa kuzidi wataalamu na wafanyakazi 400 wa usafiri wa anga katika fani hiyo.
Ikumbukwe kwamba Misri iliandaa toleo la kwanza la tukio hilo mwaka 1992 na matoleo mengine mengi katika miaka iliyopita, ya mwisho iliyokuwa mwaka 2018, na takwimu zinaonesha kuwa matoleo yaliyoandaliwa na Misri ni ya juu zaidi katika suala la ushiriki na mahudhurio katika vikao vya mkutano.