Habari

Rais Abdel Fattah El-Sisi atembelea kaburi la Mahatma Gandhi na kuweka shada la maua kwenye kaburi lake

Hotuba ya Rais wa Jamhuri
katika daftari la wageni wakubwa (VIP) wakati wa kutembelea kaburi la Gandhi huko New Delhi).

 

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, mwenye kurehemu “

Nina fahari ya kuelezea heshima yangu ya dhati katika kutembelea kaburi la kiongozi wa India marehemu, Mahatma Gandhi, aliyeashiria hatua muhimu katika historia ya binadamu kwa kujumuisha misingi na maadili ya haki, amani, usawa na kutokuwa na vurugu, pamoja na misimamo yake ya kizalendo ya ujasiri na upendeleo usio na masharti kwa chaguo la upinzani wa amani.

Dunia nzima inahitaji kuongozwa na misingi hiyo mikuu ambayo imechangia umoja na kufufuliwa kwa taifa la India, na ambayo tunaiamini na kuifuata Misri katika enzi na nyakati tofauti. Misri na India zinashiriki viunganishi vya kawaida vya ustaarabu na kihistoria na zinafanana katika dhamira yao thabiti ya kueneza usalama, amani na utulivu na kusaidia maendeleo, ustawi na ukuaji wa miji.

Back to top button