Habari

Rais wa Jamhuri ya India ampokea Rais Abdel Fattah El-Sisi

“Bi. Draupadi Mormo, Rais wa Jamhuri ya India ampokea Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi katika Ikulu ya Jamhuri ya “Rashtrapati Bhavan” katika New Delhi”

Msemaji rasmi wa urais wa Jamhuri alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya India alimkaribisha Mheshimiwa Rais, akielezea shukrani za India kwa Misri katika ngazi rasmi na maarufu, na fahari yake kwa mahusiano yenye muda mrefu yanayounganisha nchi hizo mbili rafiki.

Rais wa Jamuhuri ya India pia alisifu uzoefu wa mafanikio wa maendeleo unaoshuhudiwa nchini Misri pamoja na uongozi wa Mheshimiwa Rais katika nyanja zote na miradi mikubwa ya kitaifa inayotekelezwa sasa, akisisitiza uangalifu wa nchi yake kuunga mkono juhudi za Maendeleo za Misri na kuisaidia katika nyanja zote kupitia kubadilishana uzoefu na uwekezaji wa pamoja.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Rais alionesha shukrani kwa mapokezi makubwa ya India, akisifu mahusiano makubwa ya kirafiki ya kihistoria ya Misri na India na kiwango cha juu kilichofikiwa katika ngazi mbalimbali mnamo kipindi cha hivi karibuni, na akielezea hamu ya Misri ya kuuongeza zaidi na kuimarisha, haswa katika ngazi ya kiuchumi na kibiashara, pamoja na kuongeza kiwango cha uwekezaji wa India huko Misri.

Katika muktadha huo, Mheshimiwa Rais alisisitiza kuwa uwekezaji wa India kwa sasa una nafasi kubwa ya kuwepo katika Soko la Misri ili kufaidika na miundombinu ya kisasa nchini Misri na kupitia kwake, kufikia masoko ya Afrika, haswa kwa kuzingatia mikataba ya biashara huria inayounganisha Misri na kambi mbalimbali za kiuchumi za kikanda, akisisitiza makaribisho ya watu nchini Misri kwa kushirikiana na India, kuongeza uwekezaji wake na shughuli zake za kibiashara.

Msemaji rasmi aliongeza kuwa mazungumzo hayo yalishughulikia masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja, ambayo majadiliano yalionesha maelewano kati ya pande hizo mbili kuhusu njia za kukabiliana na masuala yote, na Rais wa Jamhuri ya India, katika muktadha huu, alisifu jukumu muhimu linalochezwa na Misri katika ngazi ya kuimarisha utulivu katika Mashariki ya Kati na Afrika, pamoja na kuunga mkono ufumbuzi wa amani kwa migogoro iliyopo mazingira yake ya kikanda.

Back to top button