Siasa

Balozi wa Misri nchini Sudan akutana na mtawala wa wilaya ya Darfur, Mkuu wa harakati ya Jeshi la Ukombozi wa Sudan

Ali Mahmoud

0:00

Balozi Hani Salah, Balozi wa Misri jijini Khartoum alikutana na “Minni Arko Minawi”, mtawala wa wilaya ya Darfur, mkuu wa harakati ya ukombozi wa Sudan na mkuu wa kamati ya uhusiano wa kisiasa ya vikosi vya uhuru na mabadiliko “makundi ya demokrasia”, ambapo mkutano huo ulijadili maendeleo ya mchakato wa kisiasa unaoendelea sasa nchini Sudan.

Balozi Hani Salah amesisitiza msaada wa Misri kwa juhudi zote zinazolenga kufikia utulivu nchini Sudan, akiashiria mahusiano ya milele na ya kihistoria yanayounganisha nchi hizo mbili, akielezea matarajio yake kwamba kipindi kijacho kitashuhudia kuhakikisha makubaliano yanayotakiwa kati ya pande zote za Sudan na kusonga mbele kwa mafanikio katika kipindi cha mpito.

Mtawala wa wilaya ya Darfur ameelezea pia fahari yake kwa juhudi za Misri nchini Sudan katika ngazi zote kufikia haraka makubaliano kati ya vikosi vyote vya kisiasa vya Sudan na sehemu zake.

Back to top button