Habari Tofauti

Waziri wa Elimu ya Juu atafuta njia za kuunga mkono ushirikiano na kampuni ya Microsoft

Ali Mahmoud

0:00

Dkt. Ayman Ashour, Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi, alikutana na ujumbe wa Microsoft ulioongozwa na Mhandisi Mirna Aref, Meneja Mkuu wa Microsoft Misri; kujadili taratibu za ushirikiano katika masuala ya pamoja kati ya Wizara na kampuni ya Microsoft, kwa mahudhurio ya Dkt. Hisham Farouk, Waziri Msaidizi wa mageuzi ya kidijitali, na Dkt. Sherif Kishk, Waziri Msaidizi wa utawala bora, katika jengo maalum la elimu huko Kairo Mpya.

Mwanzoni mwa mkutano huo, Waziri alisifu ushirikiano wenye manufaa na kampuni ya Microsoft katika sekta ya elimu ya juu, na haswa ushirikiano uliopo kati yake na Wizara ya Elimu ya Juu katika utekelezaji wa mpango wa mageuzi ya kidigitali, akisisitiza uangalifu wa Wizara wa kushirikiana na makampuni ya kimataifa na kufaidika na utaalamu wao katika uwanja huo, akielezea kwamba mwelekeo wa wizara kuelekea mageuzi ya kidigitali umekuwa hitaji la lazima kwa kuzingatia mwelekeo wa jumla wa nchi kuelekea uwekaji wa huduma zote kidijitali; kuwawezesha wananchi, kufaidika na data ya enzi ya kidigitali, na kwenda sambamba na maendeleo makubwa ya kiteknolojia katika nchi mbalimbali Duniani.

Dkt. Ayman Ashour alisisitiza dharura ya kuongeza matumizi ya huduma na programu za Microsoft zijumuishe huduma zote za elimu na utafiti kwa faida ya jamii ya kitaaluma na utafiti katika makundi yake yote, na pia kupatana na maoni ya mustakabali ya mfumo wa elimu ya juu na utafiti wa kisayansi 2022-2032.

Wakati wa mkutano huo, pande hizo mbili zilijadili mafanikio muhimu zaidi yaliyopatikana ndani ya mfumo wa makubaliano ya ushirikiano wa pamoja na kampuni ya Microsoft, mpango wa kutumia mfumo wa mageuzi jumuishi ya kidijitali kwa moja ya Vyuo Vikuu vya Misri, njia za kuhamisha uzoefu wa Misri katika mageuzi ya kidijitali ya kielimu kwa nchi za Afrika, pamoja na matumizi ya mifumo ya akili bandia katika maendeleo ya kazi ya utafiti, pamoja na mpango wa Windows kwa kila mwanafunzi wa chuo kikuu.

Kwa upande wake, Mhandisi. Mirna Aref alimshukuru Dkt. Ayman Ashour, Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi, kwa msaada wake kwa ushirikiano huu kati ya Wizara na kampuni ya Microsoft; kwa kutekeleza mpango wa mageuzi ya kidijitali katika vyuo vikuu, na kwa maoni yake ya baadaye juu ya umuhimu wa kwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia ndani ya taasisi za elimu, akiashiria kuwa kampuni ya Microsoft inajivunia ushirikiano wake na Misri kama mfano wa kuigwa barani Afrika, haswa Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi, na kwa kushirikiana na utaalamu mashuhuri wa vyuo vikuu vya Misri kama mshirika wa taasisi za elimu; kuongeza ufanisi wa miundombinu ya habari katika vyuo vikuu, akisisitiza dhamira ya kampuni ya kushirikiana na Wizara na taasisi zake zote za elimu؛ Kuendeleza ustadi wa wanafunzi, washiriki wa vitivo na mashirika ya usaidizi, kutumia uwezo wa teknolojia na kompyuta ya wingu, na kunufaika na fursa za ufumbuzi wa akili bandia ili kuharakisha ajenda ya mageuzi ya kidigitali nchini Misri.

Wakati wa mkutano huo, Amr El-Masry, Mkurugenzi wa Sekta ya Elimu kwa Afrika Kaskazini kwenye Microsoft, alitoa mada kuhusu mafanikio yaliyofikiwa na Microsoft kwa kushirikiana na Wizara katika Jukwaa la Elimu la Umoja “Egypt Hub” mnamo Mwaka wa 2021/2022, ikiwa ni pamoja na: Idadi ya watumiaji wa huduma za Microsoft (Office 365) katika vyuo vikuu vya umma Barani Afrika na Nchi za Kiarabu imefikia watumiaji 900,000, na ushiriki wa wanafunzi 2,800 katika Mpango wa Usiku wa Ramadhani kueneza ujuzi kwa wanafunzi wa chuo kikuu, na kusaidia vyuo vikuu kiufundi kupitia huduma za Microsoft Premier Services, na kusambaza vyuo vikuu vya kibinafsi, kwa mara ya kwanza katika soko la Misri, na vifaa vya Microsoft Surface, pamoja na mafunzo ya wanachuoni wa kitivo 30,000 ndani ya mfumo wa kujenga uwezo wa waelimishaji katika vyuo vikuu vya umma, pamoja na kipengele cha kuboresha mawasiliano na watu wenye ulemavu, na pia kusasisha na kuendeleza tovuti ya maombi ya kielekteroniki na mitihani ya kuingia kwa vyuo vikuu vya kibinafsi, na mengine.

Amr El-Masry aliongeza kuwa imepangwa wakati wa 2022 / 2023 kuongeza manufaa kutokana na makubaliano ya Microsoft ya elimu ya juu, akibainisha kuwa inalengwa kufikia watumiaji milioni moja na nusu wa teknolojia za (Office 365) na kutoa Windows kwa kila mwanafunzi, na mitihani kwa wanafunzi bila gharama za ziada kuhamisha ujuzi wa soko la kazi, akibainisha kuwa mashirika yanayolengwa ni vyuo vikuu vya umma, binafsi, na kiteknolojia, akipitia huduma zinazotolewa na Microsoft kwa vyuo vikuu vya umma na binafsi na mwanzoni mwa Mwaka wa 2022 / 2023, iwe kwa wanafunzi au wanachuoni, kama vile maktaba ya kidijitali inayotolewa kwa vyuo vikuu “Learning Hub” inayotoa huduma zote zilizotajwa kupitia programu kwa njia ya moja ndani ya Microsoft teams.

Waliohudhuria mkutano huo Bw. Amr El-Masry, Mkurugenzi wa sekta ya elimu kwa Afrika Kaskazini kwenye Microsoft, Bi. Noreen Fadel, mkurugenzi wa huduma za utekelezaji kwa sekta ya elimu katika Microsoft Misri, Mhandisi. Mohamed Majed ni mtaalamu wa kompyuta ya wingu katika Microsoft.

Inatajwa kwamba makubaliano ya ushirikiano yalisainiwa na kampuni ya Microsoft mnamo mwaka wa 2021 kwa lengo la kutoa huduma za (kusasisha na kuendeleza tovuti ya Wizara ya Elimu ya Juu na Utafiti wa Kisayansi kwa kuongeza teknolojia za kisasa zaidi za akili bandia kutoa huduma tofauti na kuboresha uzoefu wa kuwasiliana na watumiaji wa tovuti), na pia uwezekano wa matumizi ya wanafunzi kwa huduma za wingu za Microsoft kupitia barua pepe ya chuo kikuu kwa kila mwanafunzi, kutoa toleo la “Windows” kwa mara moja kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu vya umma kwa mpango wa Microsoft, na kutoa matoleo ya programu za (MS- Office) na toleo la barua pepe ya serikali kwa wanafunzi na wanachuoni kwa vyuo vikuu 27 vya umma na idadi ya vyuo vikuu binafsi.

Back to top button