Vijana Na Michezo

Waziri wa Vijana ajadili ushirikiano wa nchi mbili na maafisa wa FAO nchini Misri

Ali Mahmoud

Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na maafisa wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa “FAO”, kujadili ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara na Shirika hilo kuhusu mafunzo ya kilimo kwa vijana katika vituo mbalimbali vya vijana katika ngazi ya mikoa ya Jamhuri.

Mkutano huo ulishughulikia njia za ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara na Shirika hilo kuhusu uanzishwaji wa vilabu vya kilimo katika vituo vya vijana vinavyolenga elimu, mwongozo na masomo kwa vijana katika mikoa mbalimbali chini ya jina la “Klabu ya Kilimo”, kufanya kazi katika itifaki ya ushirikiano na mkataba wa maelewano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo, na Shirika la FAO na Wizara ya Kilimo katika suala hili, na kuanzishwa kwa uwanja wa kilimo katika programu ya Endeleza na Badilisha.

Waliohudhuria mkutano huo kwa upande wa Shirika la FAO, Dkt. Nasr El-Din Haj El-Amin, mwakilishi wa FAO nchini Misri, Dkt. Mohamed Yacoub, Mwakilishi Msaidizi wa FAO, Dkt. Tony Al-Atl, Mratibu wa mipango, Dkt. Dalia Aboul Fotouh, Afisa Mipango ya Kiuchumi na Vijana katika Ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Karibu na Afrika Kaskazini, Rawya Al-Dabi, Mtaalamu wa Mawasiliano, na kutoka Wizara ya Vijana na Michezo, Dkt. Abdullah Al-Batsh, Naibu Waziri kwa Sera na maendeleo ya Vijana, Manal Gamal, Mkuu wa Idara Kuu ya Uwezeshaji Vijana, na Dkt. Mustafa Magdy, Waziri Msaadizi wa Sera na Maendeleo ya Vijana.

Katika muktadha huo, Waziri huyo alisisitiza kuwa Wizara inashirikiana kwa karibu na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Misri kwa ajili ya ushiriki zaidi wa vijana na kuwawezesha, akiashiria kundi la vifurushi vya miradi jumuishi na mipango kabambe nchini Misri kwa lengo la kuwawezesha vijana katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, michezo na maendeleo, ambayo yote yanafanya kazi kwa kuzingatia maagizo ya Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.

Waziri huyo alielezea nia yake kubwa ya kushirikiana na FAO kuhusu mafunzo ya kilimo kwa vijana katika vituo mbalimbali vya vijana katika ngazi ya mikoa ya Jamhuri, ambapo mustakabali ni kwa kilimo na bima ya chakula katika mwanga wa migogoro ya kimataifa na tendo la nchi zote za dunia juu ya kujitosheleza na bima ya chakula, pamoja na utofauti wa hali ya soko na uwekezaji katika miradi ya kilimo kwa ukubwa wake mbalimbali.

Dkt. Ashraf Sobhy alitaja kuwa vijana wamekuwa na sehemu kubwa zaidi ya uungaji mkono na uangalizi wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi tangu wakati wa kwanza wa kuwajibika kwa nchi na daima kuwaweka mstari wa mbele katika safu na masuala yao, mahitaji na maombi yao yapo kichwani mwa ajenda ya kitaifa na kwa sababu ya utunzaji ule na msaada huu, wamekawa mojawapo ya malengo muhimu zaidi ya mipango ya kina ya maendeleo ambayo Misri inaishuhudia sasa.

Kwa upande wake, Dkt. Nasr El-Din Haj El-Amin, mwakilishi wa Shirika la Fao nchini Misri, alielezea furaha yake kubwa kwa mapokezi ya joto katika Wizara ya Vijana na Michezo, akielezea kuwa kufanya kazi na vijana ni miongoni mwa vipaumbele na maslahi ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa “FAO” mnamo kipindi kijacho.

Back to top button