Namira Najm: Wahamiaji Milioni 150 wa Afrika ni utajiri halisi wa kukuza sura ya bara ulimwenguni
Ali Mahmoud
Mkutano wa kupunguza gharama za uhamisho wa diaspora ya Afrika uliofanyika Rabat, Mji Mkuu wa Morocco, ulihitimishwa, Balozi Dkt. Namira Najm, mkurugenzi wa kituo cha Afrika cha uchunguzi na mratibu wa kikao cha mwisho, aliwasilisha mapendekezo ya matokeo ya kongamano yenye kichwa “mahitimisho ya Rabat”.
Najm alisema mwanzoni mwa uwasilishaji wake wa mapendekezo ya jukwaa, kwamba alitoa shukrani zake kwa Mfalme Mohamed wa Sita, mfalme wa Morocco kwa kumkaribisha kwa moyo wote, kuandaa kongamano hili na juhudi zilizofanywa kuunda hali zote zinazohitajika kufanikiwa, na kusifu ufalme wa Morocco kama nchi mwenyeji wa kongamano na Jamhuri ya Togo kwa ushirikiano wenye mafanikio wa kongamano hili.
Balozi huyo alieleza kuwa mapendekezo hayo yaliashiria kuwa diaspora ya Afrika inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 150 mnamo Mwaka wa 2021, inawakilisha utajiri halisi wa kukuza sura ya Afrika, kuthamini mizizi yake ulimwenguni, kuimarisha mabara na kuyaendeleza, kuhimiza ushiriki kamili wa wahamiaji waafrika, na kuwahimiza washirika waafrika na wa kigeni kuongozana na nchi za kiafrika katika uwanja wa kukuza uhamisho wa fedha.
Aliendelea: kukubaliana juu ya mahitimisho na mapendekezo yanayofuata kongamano kuhusu mchango wa diaspora ya Afrika katika maendeleo na kupunguza umaskini katika Afrika kupitia uhamisho wa fedha, na kutambua mchango mkubwa wa wanadiaspora wa Afrika kwa malengo ya maendeleo endelevu ya malengo ya maendeleo (SDGs), haswa lengo na. 10 miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu.
Aliendelea: kuhamasisha ushiriki wa wadau katika matukio na makongamano ya kimataifa yanayolenga kuongeza athari nzuri ya wanadiaspora wa Afrika juu ya maendeleo endelevu, kukuza ujuzi wa kifedha ili kukuza nafasi za uwekezaji katika nchi za asili, kukuza kikamilifu uhisani katika diaspora, ambayo ni aina muhimu ya mchango wa kifedha kwa maendeleo, kuhamasisha nchi za Afrika kuendeleza mipango ya kitaifa ya kimkakati kuhusu uhamisho wa fedha kuhamasisha nchi za Afrika kuangazia maeneo ya kipaumbele kuboresha urasimishaji wa uhamisho wa fedha.
Mkurugenzi wa kituo cha Afrika cha uhamiaji aliongeza kuwa kuhusu matarajio ya uhamisho wa fedha kutoka diaspora ya Afrika na mfumo wake wa udhibiti na wa uendeshaji, mapendekezo hayo yaliimarisha mshikamano na muunganiko wa sera za umma zilizoundwa na taasisi za nchi na serikali, kwa lengo la kuunganisha uhamisho wa fedha, mitaji ya uwekezaji wa wanadiaspora wa Afrika na uwezo wao wa ujasiriamali katika uwanja wa maendeleo na vipaumbele vya nchi za Afrika, kuboresha mawasiliano na kukusanya takwimu za kimkakati kuhusu mtiririko wa utumaji fedha na sifa za masoko ya Afrika kuwajulisha watoa maamuzi, kuimarisha mazingira wezeshi ya kisheria ya udhibiti na yanayohakikisha ufanisi wa soko na kupunguza gharama ya uhamisho wa fedha, kuimarisha uwezo wa serikali kutekeleza itifaki za taarifa za kuripoti mitiririko ya uhamisho wa fedha, kujenga motisha ya kifedha kwa watendaji wa umma na binafsi kutoa zaidi ya huduma za fedha na bidhaa kwa watu wasiojiweza, kuongeza uwazi wa soko kwa kutoa “watumiaji wa mwisho” na taarifa za kisasa za kiutendaji, ikiwa ni pamoja na gharama, bidhaa na huduma za kuhamisha fedha, bidhaa na huduma mpya, sehemu za kufikia, njia mpya, habari na taratibu zinazohitajika, utekelezaji wa kanuni zinazoimarisha usalama, kupunguza hatari zinazohusiana na uhamisho wa fedha, kuepuka biurokrasi yenye gharama kubwa kwa watumaji, wapokeaji na taasisi za fedha na kupanua njia ambazo huduma za benki za kiafrika zinaweza kuuzwa na kupanua wigo wa huduma za soko kupunguza gharama ya uhamisho wa fedha na kuboresha uhamisho wa fedha kutoka kwa wanadiaspora wa Afrika kufadhili nchi za bara.
Balozi Najm aliashiria kuwa kuhusu mapungufu na changamoto za kuweka huduma za kifedha katika mfumo wa kidigitali, mapendekezo yameonesha kuboresha athari za uhamisho wa fedha kupitia ujumuishaji wa kifedha na uwekezaji katika diaspora ya Afrika, kuimarisha ushirikiano wa kikanda, bara na kimataifa kati ya sekta mbili za umma na za kibinafsi na asasi za kiraia, kwa lengo la kukuza uhamisho wa fedha kutoka kwa diaspora ya Afrika, kuhamasisha watoa huduma za uhamisho wa fedha katika kutuma na kupokea nchi kutekeleza mifano ya ubunifu ya biashara na teknolojia zinazopunguza gharama za usafirishaji kwa ajili ya kufikia lengo la kimataifa la wastani wa gharama ya shughuli ya 3% kwa uhamisho wa fedha, na kukuza mazingira wezeshi kwa wavumbuzi wa kiteknolojia, kama vile biashara zinazoanza katika Fintech, ambazo zinaweza kusaidia katika kutoa huduma za kifedha kwa wakaaji ambao wanaopata ugumu wa kufikia kwake, kuunda utaratibu wa wanadiaspora wa Afrika kuwekeza moja kwa moja au kupitia zana za ubunifu katika makampuni madogo na ya kati katika sekta mbalimbali za uchumi wa Afrika, kuhimiza kubadilishana mazoea bora katika kuboresha uhamisho na uwekezaji na wanadiaspora wa Afrika kupitia benki na majukwaa ya Afrika, na kuhimiza ushirikiano kati ya sekta ya umma na ya kibinafsi ambao unahimiza matumizi ya teknolojia na uwekezaji kwa watu wanaoishi katika maeneo ya mbali ya vijijini hayana huduma, na kutoa wito kwa kamati ya Umoja wa Afrika kuwasilisha mapendekezo ya kongamano hili la “Mahitimisho ya Rabat” kwa Baraza la Utekelezaji la Umoja wa Afrika kuidhinishwa na kuwasilishwa kwa mkutano wa Viongozi wa Nchi na Serikali ya Umoja wa Afrika katika Mkutano ujao wa kilele wa Afrika.
Inatajwa kwamba lengo la kongamano, lililofunguliwa Jana na Nasser Bourita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, na Robert Doucet, Waziri wa Mambo ya Nje wa Togo, inakuja ndani ya mfumo wa kuamsha ajenda ya “Muongo ya mizizi ya Afrika na wanadiaspora wa Afrika 2021-2031”, kuendeleza mawazo ya kina juu ya hatua za kusaidia uhamisho wa fedha kwa wahamiaji wa Afrika, na kuharakisha juhudi za kupunguza gharama zinazohusiana, zasambambe na malengo ya maendeleo endelevu katika upeo wa 2030, na lengo la ishirini la mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama, uliopangwa na wa Kawaida (kufanya uhamisho wa fedha kwa haraka, salama na gharama nafuu, na kukuza ujumuishaji wa kifedha wa wahamiaji).
Washiriki wa kongamano hilo walijifunza kuunda jukwaa la biashara la kielektroniki linalounganisha wahamiaji wa Afrika na wawekezaji na wamiliki wa miradi kwa lengo la kuelekeza mtiririko wa kifedha kwa jamii za Afrika kuelekea uchumi uliojengwa, na kutumia ipasavyo uzoefu wa wananchi wa nchi za Afrika kuendeleza mifano ya ubunifu ya ushiriki wa kifedha.
Shughuli za kongamano hilo zilihusu vikao vikuu vitatu, vinavyohusiana na “kupunguza gharama za uhamisho wa fedha na mchango wa wahamiaji wa Afrika katika maendeleo na kupunguza umaskini Barani Afrika kupitia uhamisho wa fedha”,”matarajio ya uhamisho wa fedha wa wanadiaspora wa Afrika: mfumo wa udhibiti na uendeshaji”, na “Uwekaji dijitali wa huduma za kifedha na utaratibu wa ubunifu kupunguza gharama za uhamisho”.
Mapendekezo ya kongamano hilo, yanayojulikana kama “matokeo ya Rabat”, yatawasilishwa katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, unaopangwa kufanyika Februari ijayo, kwa lengo la kufikia uamuzi wa Umoja huo kuhamasisha uhamisho wa fedha kutoka kwa wanadiaspora wa Afrika kwenda bara, haswa kwa kupunguza gharama zao.