Uchumi

Waziri mkuu wa Somalia akagua Taasisi ya Afya ya Wanyama na asisitiza umuhimu wa kunufaika na uzoefu wa Misri katika shughuli mbalimbali za kilimo

Ali Mahmoud

Wakati wa ziara yake ya Sasa jijini Kairo, Bwana Hamza Abdi Berri, Waziri mkuu wa Somalia na ujumbe wake ulioambatana walitembelea Taasisi ya Afya ya Wanyama ya Kituo cha Utafiti wa Kilimo kwenye Wizara ya Kilimo na kufufua Ardhi.

Anasindikizwa na Bw. Daoud Owais Jameh, Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii, Mhandisi Mustafa Al-Sayad, Naibu Waziri wa Kilimo kwa mifugo, samaki na kuku, Balozi Elias Sheikh Abu Bakr, Balozi wa Jamhuri ya Somalia nchini Misri, na maafisa kadhaa wa Somalia.

Wakati wa ziara hiyo, “Berri” alisifu kile alichokishuhudia na kiwango cha juu cha kiufundi cha Taasisi ya Afya ya Wanyama, kwani inajumuisha kundi mashuhuri la maabara za kipekee katika eneo hilo, ambalo linazingatiwa maabara ya kumbukumbu ya kimataifa, na akasema kuwa anatarajia kufaidika na uzoefu wa Misri katika uwanja wa shughuli mbalimbali za kilimo na kuimarisha mahusiano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Akisisitiza kuwa Somalia ina utajiri wa mifugo unaokadiriwa kuwa mifugo milioni 40, pamoja na hekta milioni 8.5 za ardhi ya kilimo, akitoa shukurani kwa Serikali ya Misri kwa makaribisho mazuri na ukarimu uliopokelewa kwa ujumbe wa Somalia nchini Misri, akisisitiza kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili za kindugu ni wa milele na wa kihistoria.

Kwa upande wake, Dkt. Mumtaz Shahin, Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Wanyama, alisisitiza shauku kubwa iliyolipwa na Serikali ya Misri kwa utafiti wa kisayansi wa kilimo na msaada uliotolewa na Waziri wa Kilimo na kufufua Ardhi, Al-Sayed El-Quseir, kwa Taasisi ya Afya ya Wanyama.

“Shahin” alionesha juhudi, mafanikio na shughuli za Taasisi na jukumu lake katika kulinda mifugo, kuku na samaki, pamoja na kupambana na magonjwa ya kawaida kati ya binadamu na wanyama kuhifadhi afya ya wanyama, na kulinda afya ya wananchi.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo ni moja ya taasisi kubwa zaidi za utafiti nchini Misri, ambapo inajumuisha karibu wafanyakazi na watafiti 3000, wanaofanya kazi kupitia idara za taasisi, maabara yake, na matawi yake katika mikoa, ambayo yanafikia matawi 38 yaliyosambazwa katika ngazi za Jamhuri.

“Shahin” alisema kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na kufanya utafiti na masomo ya kisayansi, vitendo, uchunguzi na maabara kwa magonjwa ya wanyama, kuku na samaki, pamoja na kugundua magonjwa ya kigeni ambayo hayajasajiliwa hapo awali ndani ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na kutafuta njia za uchunguzi za haraka na kisasa zinazozingatia viwango vya kimataifa vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani, pamoja na kuendeleza mbinu za uchunguzi wa maabara.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo alisisitiza umuhimu wa jukumu lake katika kulinda mifugo kutokana na milipuko na magonjwa ya kuambukiza, kulinda afya ya umma na afya ya binadamu kutokana na hatari ya magonjwa ya kawaida, kuhakikisha usalama wa vyakula vyenye asili ya wanyama, pamoja na kulinda mazingira kutokana na uchafuzi na vimelea vya magonjwa, pia inafanya tafiti juu ya maendeleo na uboreshaji wa chanjo za magonjwa ya virusi na bakteria na vifaa vya uchunguzi kwa magonjwa ili kuongeza uwezo ikiwa ni pamoja na kuongeza nguvu na ufanisi wa maandalizi haya na matumizi ya chanjo zinazohitajika.

Akiashiria kuwa Taasisi ya Afya ya Wanyama imepata kibali cha kimataifa katika zaidi ya sampuli 400 tofauti za vipimo na hutoa bidhaa zenye ubora zinazoendana na viwango vya kimataifa na imepata vyeti vyote vya kimataifa na vibali katika uwanja wake wa utaalamu, na kwamba Shirika la Afya ya Wanyama Duniani limeidhinisha Maabara ya mafua ya ndege na ya Brucella kama maabara mbili za kumbukumbu Duniani kote. Taasisi hiyo pia inawakilisha Bara la Afrika katika Shirika la kimataifa nayo ni kiwango cha kimataifa katika ukaguzi wa usalama wa chakula katika Umoja wa Afrika, pia hutumikia miradi mikubwa ya kitaifa ya nchi ya Misri katika uwanja wa mifugo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Wanyama alisisitiza kuwa katika utekelezaji wa maagizo ya uongozi wa kisiasa, uwezekano wote wa taasisi hiyo ni katika huduma ya ndugu wa Afrika.

Back to top button