Habari

Balozi wa Misri nchini Sudan akutana na Waziri wa Uchukuzi wa Sudan

Mervet Sakr

0:00

Balozi Hany Salah alikutana na Waziri wa Uchukuzi wa Sudan mjini Khartoum, Bw. Hisham Abu Zeid, ambapo mkutano huo ulijadili maendeleo ya miradi ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, haswa ile inayohusiana na kuunganisha reli kati ya nchi hizo mbili na tafiti za uwezekano zinazoendelea sasa katika suala hili, pamoja na maendeleo ya gati la mto wa bandari ya “Wadi Halfa”, inayosimamiwa kwa upande wa Misri, pamoja na utekelezaji wa matokeo ya mikutano ya kikao cha kumi na mbili cha Kamati ya Bandari za Pamoja kati ya Misri na Sudan iliyoandaliwa na Khartoum Oktoba mwaka jana.

Balozi huyo wa Misri ameashiria umuhimu wa kipekee unaotolewa na Misri kwa kuimarisha ushirikiano na Sudan katika nyanja zote za usafiri wa ardhini, baharini na mtoni, kwani miradi hii ina athari chanya kwa nchi hizo mbili, iwe katika suala la harakati za watu, au kuimarisha harakati za biashara kati ya nchi hizo mbili, pamoja na athari chanya kwa nchi hizo mbili kiuchumi.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi mteule wa Sudan alisifu ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, na maendeleo chanya yanayoshuhudiwa na miradi ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, akibainisha kuwa nchi yake kwa sasa inajifunza njia za ushirikiano katika mradi wa kuunganisha ardhi kati ya Misri na Chad kupitia Sudan.

Back to top button