Mji wa Alexandria
Mji huu uko kando ya Delta ya Nile kaskazini mwa Misri takriban 225 km kutoka Kairo , eneo lake kilomita mraba 100. Idadi ya wakazi wake 3,050,000. Ni mji mkubwa wa pili nchini Misri na Afrika. Pia ni bandari kubwa katika Misri. Ulijengwa mwaka 332 kabla ya kuzaliwa Kristo na Alexander Mkuu, mfalme wa Makedonia kwa sababu kigriki wameivamia Misri. Ilikuwa ni kituo cha kisiasa, kiuchumi, kitamaduni, na biashara. hali ya hewa yake ni kupendeza ,ni mapumziko ya majira ya joto, unaojulikana kama “bibi Mediterranean.”
Jina la mji limetokana na mfalme Aleksander Mkuu wa Makedonia ya Kale aliyeunda mji huo mwaka 332 kabla ya kuzaliwa kristo .
Waptolemaio waliotawala Misri baada ya Aleksander waliufanya kuwa mji mkuu wa milki yao na kitovu cha elimu na sayansi. Maktaba ya Alexandria yalikuwa na vitabu vingi kuliko maktaba zote duniani.
Wataalamu toka pande zote za dunia walifika Aleksandria, mji wa elimu, ili kusoma na kunakili vitabu.
Pharos ya Alexandria ilikuwa mnara wa taa iliyohesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale.
Usafiri ndani ya Alexandria huenda kwa kutumia barabara, njia za reli na reli ya juu ya ardhi “Tram”. Kuna teksi na mabasi ambayo ni ya umma au ya binafsi. Njia nyingi za mabasi yanakutana kwenye El-Mawaf .
Alexandria ilipata umaarufu mkubwa kwa sababu ya wakazi wake kama mwana wa fasihi Tawfik El Hakim, mtaalamu wa fani ya ujenzi Hassan Fathi , mshairi Kostantin Kafafes , mwanamuziki Sayed Darwish , msanii Amr El Sherif , bingwa wa kuogolea Abo Hief na mtengenezaji wa filamu Yossef Shahin.
Vivutio vya Alexandria:
Nguzo ya El- Sawari
Ni miongoni wa maeneo ya kale yaliyo maarufu zaidi mjini Alexandria . iko juu ya kilima cha kale Kom El- Shakafa. Urefu wake ni takriban mita 27 . Ilijengwa mnamo karne ya tatu baada ya kuzaliwa Kristo kama ni kumbukumbu ya mfalme Diklanyos .
Jukwaa la kiroma
Lipo katikati ya Alexandria katika eneo Kom El-deka . lilijengwa mwanzoni mwa karne ya nne baada ya kuzaliwa Kristo .
Boma la Qaitbay
Iiko magharibi mwa Alexandria katika eneo Bahari . lilijengwa kuanzia tarehe 882 hadi 884 baada ya Hijra ya mtume.
Maktaba mpya ya Alexandria
Ni alama ya kiutamaduni iliyojulikana ulimwenguni kote . Iko eneo la Shatbi karibu ya bahari la Mediterranean . Inajumuisha vitabu ambavyo idadi zao ni zaidi ya milioni 8.
Chanzo: Tovuti ya Harakati ya Nasser kwa Vijana