Siasa

Misri yatoa misaada ya chakula na matibabu kwa Somalia

Mevet Sakr

Ubalozi wa Misri mjini Mogadishu ulipeleka kwa serikali ya Somalia shehena ya misaada ya kibinadamu iliyotolewa na serikali ya Misri kwa mchango wa Al-Azhar Al-Shareif, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Afya na Idadi ya Watu, Wizara ya Mshikamano wa Kijamii na Hilali Nyekundu ya Misri kwa uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, na msaada huo uliwasili kwa njia ya bahari mjini Mogadishu kwa jumla ya tani 240 za chakula, matibabu na vifaa vya msaada.

Shehena ilikabidhiwa kwa mahudhurio ya Balozi Mohamed El-Baz, Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri mjini Mogadishu, na Dkt. Ali Haji Adam, Waziri wa Afya wa Somalia, na baadhi ya maafisa wa serikali ya Somalia, na wawakilishi wa Hilali Nyekundu ya Somalia. Hii, na usafirishaji wa msaada wa Misri kwenda Somalia katika muktadha wa mahusiano mashuhuri kati ya nchi hizo mbili, Na ari ya uongozi wa kisiasa wa Misri kuunga mkono serikali ya Somalia na watu kukabiliana na wimbi la ukame Somalia imelokuwa ikikabiliwa nayo kwa miaka kadhaa.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya wa Somalia alitoa Shukrani zake kwa serikali ya Misri, akisisitiza mahusiano ya kindugu kati ya nchi hizo mbili na umuhimu wa misaada ya Misri kuchangia katika kukabiliana na ukame, Pamoja na nia yake ya kuimarisha ushirikiano na Misri katika nyanja ya afya na mafunzo ya wafanyakazi wa matibabu.

Back to top button