Maeneo Ya Kihistoria

Makumbusho ya kitaifa ya Aleskandaria

0:00

Ni miongoni mwa Makumbusho ya Aleskandaria na yako karibu na njia ya uhuru

 Ni kama  jumba la zamani la mfanyabiashara mmoja tajiri  wa mibao aliiitwa “Asaad Basili”aliyeyajenga kama majengo ya kiitalia.Mnamo 1954 Makumbusho yameuzwa kwa Ubalozi wa kimarekani  kwa kiasi Cha paundi za kimisri elfu 53.na Baraza kuu la mabaki ya kale limeyanunua kwa kiasi cha paundi milioni 12.na ambalo limeyabadilika kuwa Makumbusho ya kitaifa kwa mji, baadaye Rais wa zamani Mubark akafungua Septemba mosi 2003.

 Jumba la makumbusho lina zaidi ya  vipande vya kale 1800 vinavyoashiria vipindi vyote tangu kipindi cha taifa la kale hadi kipindi kipya , na vipande hivyo vinaonesha Ustaarabu wa Misri , Utamaduni,Sanaa,na Utengenezaji wake wakati huo, pia vinaweza kuonesha umoja wa kihistoria na wahusika wamisiri kupitia mabaki ya kale ambayo yanatafsiri historia ya kimisri kutoka matukio ya kitaifa.

 Kwanza ,kipindi cha kimisri cha Mafarao kikizingatiwa Ustaarabu kale Sana baadaye zama ya Ptolematic , zama ya kirumi , Bizinti na kiislamu na mwisho wa vipindi hivyo kwa familia ya Mohamed Ali na mwisho wake kwa mapinduzi ya 1952.

Na vipande hivyo vimekusanyika kutoka  majumba mengi miongoni mwa majumba hayo, jumba la kimisri ,la kiislamu ,la kikoptiki mjini Kairo .na jumba la makumbusho la kigiriki , kirumi na mabaki ya kale yaliyozama na mabaki ya kiislamu mjini mwa Aleskandaria.

  Vipande muhimu vinavyopatikana ni kama:

Sanamu la katibu mmisri na kundi la vyombo ambavyo viko kwenye Piramidi ya mfalme wa “Zousir”.

Katika enzi ya Kati kundi la masanamu yanayoashiria kubadili sanaa kutoka udhanifu hadi uhalisi .na dalili hizo huonekana wazi katika sanamu la mfalme “Amn MEHAT wa tatu”.

Ama enzi mpya  ya kitaifa imezingatiwa enzi ya kisanaa zaidi kwani kusanya baina ya uhalisi wa shule ya Tiba  na  udhanifu wa shule ya MNf, basi tulikuwa na vipande vizuri zaidi,ambavyo viko katika jumba hili kama kichwa Cha mfalme” HATSHEPSUT “na kichwa Cha mfalme EKHNATON.

Na kundi la kisanaa la mfalme “TOHTMS” wa tatu wa Mungu Amon na mfalme wa Ramses wa pili.

Katika enzi ya kabla ya enzi ya mwisho aidha iko kundi la sanamu kwa wafalme wa enzi hizi  na mfano wa kaburi inajumuisha sanamu ,kundi la majeneza na hirizi mbalimbali.

 

Ama sehemu ya kigiriki ya kirumi iliyojumuisha mabaki ya kale kutoka enzi mbali mbali kama Calhillenssee ,kirumi na kigiriki.

Jumba la Makumbusho ya kitaifa ya Aleskandaria ni la kipekee katika kuonesha ukumbi maalum wa vitu vya kale vilivyozama, ambavyo ni pamoja na mkusanyiko mzuri wa vitu vya kale vilivyozama ambavyo vimepatikana, na sehemu hiyo pia inaonyesha picha wazi za shughuli za uchimbaji ili wote waweze kuunda mtazamo wa sura na hali ya zamani kabla ya kupatikana.Miongoni mwa vipande muhimu zaidi katika sehemu hii ni sanamu la itale  nyeusi kwa Isis, sanamu la Kuhani mmoja wa Isis na kikundi cha masanamu ya marumaru na picha za miungu kadhaa ya Uigiriki, pamoja na sanamu la Venus, mungu wa kike wa upendo,kichwa wa mkuu wa Alexander AlAkbar na wengine.

  Ama sehemu ya tatu kutoka sehemu za makumbusho Ina enzi tatu nazo ni: enzi ya kikoptiki, kiislamu,na kisasa.

Na  sehemu ya kikoptiki inajumuisha zana zilizotumiwa katika maisha ya kila siku na zana hizi ni kutoka shaba ,fedha na pronzi .

Aidha vitu kama mibao ya hali ya kidini kama, Mbao wa Yesu na karamu ya mwisho na aidha kundi la kitambaa Cha pambma ,kitani na sufu na kundi la zana za kifahari zilizotumiwa kila siku .

Na Kuna aidha mahali kwa pesa palipojumisha pesa kutoka makundi ya enzi tofauti miongoni mwa pesa zilizokuwa chini ya maji katika ghuba ya Abu Qir .

Makundi ya pesa nyingine za enzi ya Byzantine na kiislamu .na pale Kuna kundi la silaha za enzi ya kiislamu na aidha kundi la  Maadini, glasi, na pambo zinazorudishwa  kwa enzi  tofauti za kiislamu.

Ama sehemu ya kisasa  Ina kundi mbalimbali kutoka vitu vya familia ya Mohamed Ali kutoka fedha , dhahabu na vito vya thamani vilivyokuwa vikitumiwa na  wafalme na Maamiri wa familia kuu.

Check Also
Close
Back to top button