Maeneo Ya Kihistoria

Chuo kikuu cha Al-Azhar ..Chuo kikuu kikubwa zaidi Duniani

Kimeanzishwa kabla ya Chuo kikuu cha Polonia huko Italia, pia kinazingatiwa chuo kikuu cha tatu cha zamani zaidi baada ya vyuo vikuu vya Al Zaitunah na um Al Qura, lakini wakati wote kimebaki taasisi ya kielimu wakati ambapo taasisi mbili zile zimeacha jukumu lao kama taasisi za kielimu, nayo ni Taasisi ya kidini, ya kielimu, ya kiislamu, ya kwanza na kubwa zaidi Duniani, na hupatikana mjini Kairo, Mji mkuu wa Jamhuri ya Misri ya kiarabu pamoja na matawi yake katika mikoa tofauti mengi ya kimisri .

Chuo kikuu cha Al Azhar ni mwelekeo wa waislamu wa kitaalam tangu zaidi ya miaka elfu moja ambapo ni mnara wa elimu  na mwelekeo kwa wanafunzi wa kila mahali ili kujifunza elimu za kidini , kiarabu na sayansi ya asili na ya kibinadamu , na kinabaki katika historia ndefu yake kuwa kituo cha wepesi na msimamo wastani na kueneza utamaduni wa kiislamu  , utaalam wa kiislamu na  mafundisho ya  uvumilivu vyake yasiyojua kutia chumvi au ukali , msimamo mkali au kushikia kibaya wa kimadhehebu  na kisiasa … Na kwenye viwanja vyake wafalme , masultani , marais , masheikh wa Al-Azhar , mufiti, mawaziri , mabalozi , wataalam na wengineo  kutoka maeneo ya ulimwenguni wamepata elimu.

 Chuo kikuu na Msikiti :

Chuo kikuu cha Al-Azhar kilirithi Msikiti wa Al-Azhar unaorejea historia yake kwa zama ya Fatimi ambapo Ghawhar El-Sakaly aliweka jiwe la msingi kwa amri ya khalifa Al-muizz li din Allah El-fatmy mnamo  Ramadhani 14 mwaka wa 359 AH (971AD) na Al-zahar iliteuliwa kama msikiti rasmi ambapo ulianzishwa na nchi kwa kuwa mnara wa uhubiri wa kidini na Alama ya utawala wake na msikiti huo ulifunguliwa kwa sala kwa mara ya kwanza mnamo  Ramadhani 5 mwaka wa 361 AH na uliitwa kwa jina la Msikiti wa Al-Azhar kwa ajili ya bibi Fatma Al-zahra _ Mwenyezi Mungu amuwie radhi_ ambaye wafatmeen wanazingatiwa kuwa pamoja naye.

  Na lengo la  kuanzishwa kwake mwanzoni  ni kuhubiri kwa madhehebu ya  kishia na haikupitii muda mrefu ila ukawa  chuo kikuu cha kueneza madhehebu ya kisunna ambapo wanafunzi hupokea taaluma mbalimbali za kidini na kimantiki na shukurani ya kupa  Al-Azhar jukumu la kitaalam inarejea kwa waziri Yaqub bn Kals ambapo alimshauri khalifa El-azizz mnamo mwaka wa 378 AH kuubadilisha  kwa chuo cha masomo baada ya vyuo kuwa kwa ibada ya kidini tu na kueneza madhehebu ya kishia .

Masomo yalianza kweli kwenye msikiti wa Al-Azhar mwishoni mwa enzi ya Al-muizz li din Allah Al-Fatmy  wakati jaji  Abu El hassan bin  namaani Al-maghribi alipokaa  mwaka  wa 365 hijira ( Oktoba 965 BK ) katika kikao cha kwanza cha kitaalam kisha vikao vya kielimu viliendelea baada ya hapo .

 Na vikao vya elimu vilikuwa msingi wa masomo katika Al-Azhar ( chuo kikuu na msikiti ) ambapo mwalimu anaketi ili kusoma somo lake mbele ya wanafunzi wake na wasikilizaji wanaomzungusha. Vilevile , wataalam wa dini wanaketi katika mahali wanapopewa kutoka maeneo yake . Na  mwalimu haruhusiwi kufundisha ila baada ya kuruhusiwa na porofessa wake kulingana na mfumo wa mtihani wa mazungumzo katika mada kumi na moja  na ruhusa ya kufundisha hutolewa na khalifa .

Al-Azhar ( Msikiti na chuo kikuu ) katika mfumo wake wa kielimu  ni ya kwanza  inayovumba mfumo wa mwanachuoni ulimwenguni kote na kazi ya mwalimu msaidizi  huyu ni  kurejea  tena yale yaliyosemwa na mwalimu kwa mwanafunzi . Na inapaswa kwa mwanafunzi anayetaka kufundisha ni kupitisha mtihani na kabla ya hayo kupendekezwa  na wataalamu  wawili  miongoni mwa wataalam wakubwa wa Al-Azhar tukufu . Ikiwa akipendezwa na  akipata tazkia kutoka kwa wataalamu wawili atatoa ombi pamoja na  wasifu wa sheikh wa  Al-Azhar katika historia yake halafu sheikh wa Al-Azhar akaunda kamati ina wataalamu 6 wanaoongozwa na sheikh wa Al-Azhar na inaongezeshwa kwao mwanachama mwengine   kama mwanafunzi anataka kufanya mtihani katika madhehebu ya El-Hanbaly na uamuzi wa kamati unatolewa na sheikh wa Al-Azhar ambapo kila madhehebu mmoja inawakilishwa na  masheikh wawili , na mtihani huo ulikuwa ukifanyika midomoni na hauainishwi na wakati maalum , basi mwanafunzi anafanya mtihani katika mada kumi na moja siyo vitabu kumi na moja anavikumbuka vizuri midomoni , kama akieleweka vizuri ataruhusiwa kuwa mwalimu kuanzia  muhadhara wa tatu yaani atakuwa mwalimu msaidizi kisha atapishwa baadye ili akawa mwalimu kuanzia muhadhara wa pili .

 Chuo kikuu cha Al-Azhar kilitoa katika tarehe hiyo yale yanayoshindana na vyuo vikuu kutoka mfumo wa masaa ya elimu zaidi na kumpa masomo kwa zaidi ya mwalimu moja  na mwanafunzi anaweza kuchagua na ilipatikana mhusika zaidi ya moja kwa kila mada na mwanafunzi ndiye anamchagua sheikh wake bila ya kumlazimisha kukaa hapa au pale … Hivi ndivyo mafunzo ya hiari yalikuwa huku kwenye chuo kikuu. Vilevile , mafunzo ya mtihani wa mazungumzo nayo ni mtihani bora zaidi .

 Anayefikiri kwamba ukale wa chuo kikuu cha Al-Azhar haukurejei kwa  mwaka 972 hijira na unarejea kwa mwaka 1920 anakosa kwa kiasi kikubwa, kwani uamuzi wa agizo la kifalme  unakuja katika mfumo wa kihistoria  wa kuendeleza  elimu katika Al-Azhar ambayo ni jambo la kawaida kuiendeleza katika kila kipindi .

 Wataalamu wa Al-Azhar wanafanya kazi  zao za kufundisha vizuri na hawafundishi elimu ya kidini tu bali walifundisha falsafa , Mantiki , hisabati na matibabu japo kwa kiwango kidogo  mwanzoni mpaka ElHakm b Amri allah  alianzisha  ” nyumba ya hekima ”  na wanawake walihudhuria masomo kadhaa  . Hivi karibuni masomo yalipanuka hadi  yalijumuisha  Elimu ya  unajimu , Hesabu , Matibabu , ujenzi , kijiolojia , Historia na Elimu za kijamii kadhaa na elimu mbalimbali nyinginezo . Na kuhusu wataalamu mashuhuri  ambao majina yao yaliambatana na Al-Azhar ( msikiti na chuo kikuu) ni :- Bn Khaldun , Ibn Taghri Bardi ,Musa Bin Maimon, Al Hassan Ibn Al Haytham , Muhammed Ibn Yunus Al Masry , Al Qalqashandi na wataalamu wengine  walitoa matunda ya utaalam kwa duniani kote ambao  umenufaisha utu hadi leo.

Ingawa kuwa hotuba ya Ijumaa ilisitishwa kufanyika kwenye msikiti wa Al-Azhar kwa takribani miaka mia moja wakati wa enzi ya kiayubia ila kuna ushahidi wa kuendelea masomo huku wakati mwingine . Shukrani ya kurudisha hotuba kwake chini madhehebu ya kisunna inarejea kwa sultani El Dhahir bebars  Al-bandaqady ambapo aliujenga upya  na kuurekebisha  hapo hapo  Al-Azhar  ilirejesha nafasi yake kama kuwa ni chuo kikuu cha utaalamu ambacho kina uthamini mkubwa huko Misri na ulimwengu wa kiislamu .

Enzi ya Mamluki inazingatiwa kuwa mojawapo ya enzi zinazojipambanua  kwa Al-Azhar (msikiti na chuo kikuu ) ambapo ilisifika ilichukua nafasi yake kama kituo cha elimu , na iliongezekwa kwa maktaba na vitabu vyenye thamani mpaka maktaba yake yakawa mojawapo  ya maktaba kubwa zaidi  katika mashariki na duniani kutokana na uthamini na vito  inavyo na ujenzi wake unaendelea kufanywa na masultani na wamamluki  mpaka ikawa shule kuu mjini Kairo  , na chuo kikuu kikubwa cha kiislamu  ambacho hakishindani na chuo kikuu kingine ulimwenguni  kote mwa kiislamu .

Ingawa uzembe na uthabiti uliobandisha elimu na fanii nchini Misri chini ya utawala wa kiuthumani  ila  kwamba chuo kikuu kinaendelea kuwa mahali  pa Amani , elimu na maarifa . Vilevile , Al-Azhar  ( Msikiti na chuo kikuu ) ilisimama mbele ya mapinduzi katika kipindi cha kampeni ya kifaransa nchini Misri , ambapo iliuunga mkono raia ili kumchagua Muhammed Ali kuwa mfalme wa Misri . Katika miongo hii mirefu , chuo kikuu kilikuwa chanzo pekee cha kufundisha sayansi na kuhitimu wafanyakazi na walimu wa nchi  katika ulimwengu wa kiislamu .

 Na katika zama ya kisasa pamoja na maendeleo yaliyotolewa na Muhamed Ali kulikuwa  wanafunzi na wanahitimu  wa chuo kikuu hicho  tu ili wawe kiini cha taasisi mbalimbali za elimu zilizoanzishwa ili ziwe  vituo vya elimu kwa mtindo wa kisasa wa ulaya . Vilevile , kilikuwa kiini cha ujumbe wa kielimu kwa ulaya  ili kusambaza maarifa ya kisasa .

Mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini , chuo kikuu cha Al-Azhar kilishuhudia mwanzo wa kurekebisha na kujenga upya lengo lake kukigeuza  kwa taasisi yenye mfumo wa kielimu unatumia mtindo wa kisasa , Wataalamu kadhaa waliongeza urekebishaji huo na wa kwanza wao ni Muhammed Abdu ambapo alipounda baraza la usimamizi la kwanza kwa taasisi hiyo katika Rajab mnamo 6 , mwaka wa 1312 hijira  hii ilifuatiwa  na kutolewa kwa sheria namba 10 kwa mwaka 1911 ambayo ilipanga masomo na iliyafanya kuwa  awamu  , iliweka mfumo kwa wafanyakazi , masharti ya kukubali wanafunzi na mfumo wa mitihani na vyeti , pia alianzisha  taasisi inaisimamia inayoitwa baraza kuu la Al-Azhar .

Kwa mwendelezo wa kukuza taasisi hii ya kifahari , sheria ya namba 49 kwa mwaka wa 1930 ilitolewa ambayo kulinagana nayo Vitivo vya  vitatu vya Al-Azhar vilianzishwa , navyo ni Vitivo  :-  Misingi ya dini , sheria na lugha ya kiarabu , na sheria hiyo ilielezea  uwezekano wa kupanua katika kuanzisha vyuo vikuu vingine .

 Vilevile , sayansi zisizo kisheria ziliingizwa katika vyuo vya Al-Azhar kama :- Hesabu , sayansi na masomo ya kijamii ili kuwezesha wahitimu wanapoingia kwenye Vitivo vya Al-Azhar mbalimbali , kisha sheria ya namba  26 kwa mwaka  wa 1936 ikafuata ambapo iliundwa upya nafasi ya nne nayo ni masomo ya juu na mwenendo huo ulifikia kilele  kwa sheria iliitwa  ” sheria ya maendeleo ” ilitolewa tarehe Julai 5, 1961 chini ya namba 103 kwa lengo la kuandaa tena  Al-Azhar  na kwa mujibu wa sheria hiyo , ilifanyika kazi ya chuo kikuu cha Al-Azhar kwenye uwanja wake ambacho kinajumuisha kwa mara ya kwanza Vitivo vya elimu kadhaa  kama :- biashara , matibabu , uhandisi na ukulima. Vilevile , kilifunguliwa milango ya masomo kwa  msichana mwislamu kws kujenga chuo cha wasichana kinachojumuisha sehemu za kusoma matibabu , biashara , sayansi na masomo ya kiarabu,kiislamu na masomo ya kibinadamu . Vyuo vya kisasa na kisayansi kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar vinajipambanua kuliko  vitivo vingine kwa kutilia maanani kwake  masomo ya kiislamu pamoja na masomo maalumu .

 Mifumo ya elimu katika chuo kikuu ilipanuka  na haikuishii kwenye mipaka ya mahali na wakati bali ilipelekea  kwa upande mpya  na  kisasa na ujumbe wake  hauishii kwa mawaidha , kuongeza na kufundisha tu bali uligusa pande mbali ili kiwe na uongozi katika utafiti , huduma ya umma ya kiislamu , kutetea masuala yake na kueneza kiislamu chenye msimamo wastani kwa lengo la kukabiliana na makundi ya ukatili na yenye misimamo mikali ulimwenguni kote .

Utoaji wake bado unaendelea na kwa wengi  na unaendelea kwa ujumbe  wake wa nje  na wajumbe wa tamaduni zake  wanaokwenda  nchi mbalimbali za Afrika , Ulaya , Marekani   Asia na bara la Australia baada ya kuweka wakati historia ndefu yake misingi ya mifumo na  desturi za chuo kikuu zinazojulikana na kuzitekelezwa katika vyuo vikuu duniani .

Sifa za mhitimu wa Al-Azhar

Chuo kikuu cha Al-Azhar kinajivunia kwa vitivo vya Sayansi kama ujivuno wake kwa vyuo vya kidini  kwani vina jukumu kubwa ambapo vinawafundisha wanafunzi sayansi ya ulimwengu pamoja na mafunzo ya dini  ili wabebe  ujumbe wa Al-Azhar kwa wanabiadamu pahali popote wanapokaa .

 Ujivuno huo ulitegemea  historia ndefu ambapo mwanasayansi wa macho anayejulikana ” Al-hassan bin Al- Haytham  alisoma katika Al-Azhar , Muhammed bin Yunus El-masry aliyefariki dunia mwaka 1009 mvumbuzi wa trigonometry ” Hesabu pia alisoma katika Al-Azhar . Vilevile ,  Al-Azhar ilikuwa imepokea  wataalamu wasio waislamu Ili kufundisha huku kama  msomi maarufu wa kiyahudi ” Musa Bin Maimon” ambaye aliishi huko nchini Andalusia .

 Kwa hivyo kufundisha sayansi za vitendo na majaribio zilianza katika Al-zahar mnamo tarehe ile ile ya kufundisha sayansi za kiarabu na kidini pamoja na makundi ya wahitimu wa kwanza yalikuwa huko Abu Zaabal  na idadi yao ilikuwa wanafunzi mia moja  wote ni wanafunzi wa Al-Azhar ambapo matibabu nchini Misri ilijulikana kupitia wanafunzi wa Al-Azhar .

Na wakati  huo Muhammed Ali Pasha alipotaka kutuma ujumbe wa elimu ili kuimarisha Misri , hakukuta yoyote isipokuwa taasisi ya Al-Azhar kwa hivyo jumbe tisa za elimu zilitoka kukwenda Italia , Ufaransa , Australia , Uingereza , Urusi na nyinginezo , na  zaidi ya 70% ya wanachama wa ujumbe  walikuwa Wanafunzi wa Al Azhar .. hawa ambao waliorudi  Misri na walianzisha shule ya Al-Alsun ambayo ilikuwa baada ya hivyo chuo cha Al-Alsun .

 Vilevile, walianzisha harakati za tarjama na shule ya kiufundi ya kijeshi  na nyinginezo .

 Na aliyewapendekeza wale ni Sheikh Hassan Al-Attar aliyeandika juu ya unajimu , hesabu  na Jiografia na alikuwa sheikh wa Al-Azhar , na sheikh Al-damanhory aliyetunga zaidi ya vitabu 6 katika matibabu na elimu ya anatomia  pia alikuwa sheikh wa Al-Azhar na alikuwa akiandika juu ya misingi ya sheria kama alivyoandika juu ya anatomia .

Kwa hivyo chuo kikuu kikuu cha Al-Azhar kilikuwa kimebeba njia za kuangaza na viongozi wa maendeleo ya nchi ya Misri ya kisasa  kwani  ndicho kama kiongozi wa  kuelimisha kila mahali ulimwenguni mwa kiislamu na kila wakati kwa kiwango kinachopita kiasi wakati wake daima

 Na mnamo kipindi chake chote , wahitimu wake walikuwa kutoka vijiji vya Misri na ulimwengu  na katika miji ya Misri na ulimwengu pia , watu  wa matabaka na mahali mbalimbali wanawaelekea kwake ili kutunzwa na kufaidiwa kwa utaalam wao.

Nafasi zinazopatikana na uwezo wa ushindani kwa chuo kikuu cha Al-Azhar

 Na wakati wa kuzungumzia nafasi zinazopatikana na uwezo wa ushindani kwa chuo kikuu cha Al-Azhar ndiyo pekee  nayo ni nafasi  ya kisasa kwa chuo kikuu cha Al-Azhar tu kwani Al-Azhar kinahitajikwa  wala hakihitaji  na kwa uchache utakuta taasisi inayohitajikwa wala haihitaji lolote .. na chuo kikuu cha Al-Azhar kinajipambanua  kuliko  taasisi yengine duniani kwamba ndicho kinajumuisha wanafunzi  wageni  kutoka nchi 107 , na haipatikani taasisi ya elimu duniani inakusanya  jinsia na rangi mbalimbali hizo kutoka nchi hizo isipokuwa chuo kikuu cha Al-Azhar  na ukaribisho wake kwa wageni kwa gharama ya Al-Azhar umezidi  zaidi ya miaka mia tano na hiyo miongoni mwao fursa zinazopatikana .

 Vilevile , wahitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar wanahitajika kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni na hiyo miongoni mwa  uwezo wa ushindani .

Idadi ya walimu wote kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar  inafikia  walimu 15155 na wafanyakazi wa idara kwenye chuo kikuu ni wafanyakazi 13074 , hawa wote wanahudumia takribani wanafunzi wa kiume na wa kike 500000  na miongoni mwao wanafunzi  wageni .

Katika chuo kikuu kuna  vitivo  vya vitendo 23 miongoni mwao vitivo vya kurudia   na hilo linakisukuma kutoka mashindano kwa uongozi na kutofautisha na vyengine .ikiwa kwa mfano chuo kikuu chochote kina  kitivo cha matibabu kimoja  wakati huo huo chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo vya matibabu 40 .  Na ikiwa chuo kikuu chochote kina kitivo cha sayansi kimoja , chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo vya sayansi 30. Na ikiwa chuo kikuu chochote kina kitivo cha uhandisi kimoja , basi chuo kikuu cha Al-Azhar kinajumuisha  vitivo vya uhandisi 3 ,  Ama chuo kikuu chochote kinajumuisha kitivo cha ufamasia kimoja , chuo kikuu cha Al-Azhar kinajumuisha vitivo 3 vya ufamasia  na kuna kimoja chini ya ujenzi  huku Luxor , na ikiwa  chuo kikuu chochote kina matibabu ya meno kimoja basi chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo 3 vya matibabu ya meno  na kuna kimoja kinajengwa sasa huku Luxor. Hayo yote yanaonesha uwezo wa ushindani wa chuo kikuu cha Al-Azhar hata katika upande wa vitivo vya vitendo.

Na ikiwa vyuo vikuu vingine vina hospitali moja basi chuo kikuu cha Al-Azhar kina hospitali 6 na kinatoa huduma ya matibabu kwa hadhira mara sita dufu inavyotolewa na chuo kikuu kingine .

Hayo yote yanaweka uwezo wa ushindani mbeleni  kwani kina kisichopatikana katika  chuo kingine bali kina hospitali ilifunguliwa  hivi karibuni upana wake mita za mraba 124000 nayo ni hospitali kubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya kati na ndani yake uwanja wa ndege .

Mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar na sifa za wahitimu

Sifa za mhitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar zinazomfanya  ashindane na mhitimu yeyote wa vyuo vikuu vya ulimwengu  kwa sababu mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar inategemea misingi mitatu haipatikani katika taasisi ya utaalam mwengine  ulimwenguni kote :

Kwanza :-

Chuo kikuu kinawafundisha wanafunzi wake elimu zinazonunuliwa yaani Quran tukufu na sunna .

Pili :-

Kinawafundisha elimu  zinazotumika akili kama  sayansi za machine  zinazomfundisha mwanafunzi kuelewa  vizuri kutokana na hayo mwanafunzi wa Al-Azhar. Anaelewa matini  kwa  maana kadhaa si maana moja . Ama anayesoma elimu zinazonunuliwa  tu hatumii isipokuwa maana moja tu  ili kutomkosea mwengine au kumkafirisha mtu kutoka dini   na hayo hayapatikani katika Al-Azhar tukufu  .

Tatu:-

 Chuo kikuu kinawafundisha wanafunzi wake sayansi  za vitendo-  pamoja na elimu za kisheria na kiarabu – kwa hivyo mwanafunzi anakua mwenye busara   ambapo akili haigombani na  kunukuu na dini haigombani na  dunia  kutokana na hayo ikapatikana utofauti wa madhehebu .. na kumkubali fikra za mtu mwengine nchini Misri .

 Kwa hivyo tunaona kwamba misimamo tofauti na kukubali fikra za mtu mwengine  ni miongoni mwa sifa za Mtaala wa Al-Azhar ambapo tunaona katika nyumba moja mtu anayemwabudu Mwenyezi Mungu kwa madhehebu ya El-hanafy na mwengine kwa madhehebu ya El-shafy na wa tatu kwa madhehebu ya El-malaky  bila mtu yeyote kumkasirisha mwengine au kumkosea .

Njia hii ya kufundisha kupitia elimu zinazonunuliwa , sayansi zinazotumika akili  na sayansi ya dunia inaiunda akili inaweka kuelewa vizuri na inaweza kusambamba na maendeleo kutokana na hayo wahitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar wanafundishwa ujumuishaji katika sheria ya matini na kufundishwa kwamba sayansi zinazotumika akili ni chombo kinachowezesha kufahamu  vizuri matini zinazonunuliwa  .

Mwanafunzi anasoma Mtaala mpya katika vitivo vya kisheria nao ni :- “masuala ya kisasa ”  unaogusa masuala mapya yote na utafiti wa kisayansi unaoandikwa katika chuo kikuu ambao unajadili masuala haya .. pia tulikua kujua katika Al-Azhar  kwamba kisheria inaandikwa katika kila kipindi na inapaswa kuandika katika kila kipindi , sheria inakifaa . Vilevile , chuo kikuu kinaamini kwamba  matini ni maalum na matukio hayana kikomo  yaani lazima matini ziguse masuala na matukio mapya yote .

Kwa hivyo chuo kikuu kinaendelea kuwalea wana wake juu ya Mtaala wa busara na inasimamia zaidi ya miaka elfu moja .. na ulimwengu mzima ulikipokea kwa  ukaribisho  kwa hivyo mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar inabaki kuwa urithi wa kweli kutoka urithi wa Mtume S.w na kupitia mitaala hiyo , ulimwengu ulielewa  uthamini wa njia ya kiislamu  “ujumbe na mtume ”  kwa mtindo wa mitaala hiyo, wana wa dunia walitambua historia ya umma yetu , ustaarabu wake na wanaume na mashujaa wake walioifanya maendeleo . Vilevile,  Imechukuliwa vigezo vya kweli  kutoka elimu za Al-Azhar na chuo kikuu chake ambavyo  watu wanapima vitendo vya maisha kupitia kwake na wanaelewa kipimo cha mema na mabaya sio katika  upande wa mwenendo wa mtu  tu bali kipimo cha mema na mabaya ya ustaarabu , tamaduni kwa mataifa , watu na jamii za wanadamu .

Chuo kikuu cha Al-Azhar kinabaki kuwa chanzo cha kisayansi na kielimu kwa waislamu na wengine kwa linaliambatana na elimu za kiislamu , lugha ya kiarabu na nyingine za kijamii na kibinadamu , na ambacho kiliweza kupitia hisa  yake ya kisayansi  , kielimu na kitamaduni  pamoja na hisa yake kutoka utafiti wa elimu kutoa  masuluhisho bora kwa matatizo yanayotishia jamii za kibinadamu  katika nyanja zote tofauti.

Check Also
Close
Back to top button