WAZIRI MKUU AZINDUA MITAMBO YA KISASA YA KURUSHIA MATANGAZO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekagua na kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam Media Limited.
Vifaa hivyo ni pamoja na Magari ya kisasa ya kurushia matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi viwanjani (VAR).
Vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na Zanzibar pamoja michezo mingine.
Akizungumza na wafanyakazi wa Azam Media pamoja na wadau wa michezo Mheshimiwa majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha ligi kuu ya Ufaransa (Legue 1) na ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga)