Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Sherif Abdelhamid Imam Ismail mara baada ya kuwasili Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Februari, 2023.
Pia Rais Samia amefanya mazungumzo na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Sherif Abdelhamid Imam Ismail mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho. Na katika mazungumzo yao walisisitiza kuendelezwa kwa ushirikiano katika Sekta ya Elimu Ulinzi na Uwekezaji kwenye Kilimo.