Utambulisho Wa Kimisri

Dkt. Khaled al-Anani

Khaled al-Anani amezaliwa mnamo Machi 14, 1971, katika Mkoa wa Giza, alipata shahada ya kwanza ya Mwongozo wa Kiutalii kwa Kifaransa kutoka Kitivo cha Utalii na Hoteli – Chuo Kikuu cha Helwan mwaka 1992, kisha akawa mwanachuoni, kisha akapata digrii ya Uzamili mnamo 1996, tena akapata Diploma ya mafunzo ya Egyptology mnamo 1998  kutoka “Chuo Kikuu Paul Valerie Montpellier” huko Ufaransa, na mwaka wa 2001 al-Anani alipata Uzamivu katika Egyptology kutoka Chuo Kikuu hicho hicho.

Dkt. Khaled al-Anani alifundisha katika programu tofauti ya Uzamili ya “Utalii Shirikishi” katika Chuo Kikuu cha Helwan na Chuo Kikuu cha Italia cha Palermo kati ya miaka ya 2007 na 2008, na pia katika programu ya  Uzamili ya “Kuhifadhi Urithi wa Kiuchumi” inayoshirikishwa na Chuo Kikuu cha Helwan na Chuo Kikuu cha Brandberg cha Teknolojia ya Ujerumani kati ya mwaka wa 2013 na 2015, tena akasimamia na kujadili tafiti nyingi, kufundisha katika kozi ya Uzamili ya Uhifadhi wa Urithi na Usimamizi wa Tovuti BTU, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Brandenburg, Cottbus, Ujerumani, pia alifundisha katika programu ya Uzamili “Kozi Jumuishi ya Utalii wa Mahusiano na Mipango ya Kikanda, Chuo Kikuu cha Palermo”.

Dkt. Khaled al-Anani alishikilia nyadhifa kadhaa, zikiwemo:

Mwanachama wa mradi wa Misri-Finland “EAIS”; kutengeneza hifadhidata ya mambo ya kale ya Misri mnamo kipindi cha (2004-2005).

Mwanachama wa heshima wa Jumuiya ya Misri ya Optometry tangu 2006.

Profesa Mgeni – J. Paul Valerie Montpellier 3 – Ufaransa mara saba mnamo kipindi cha (2006 – 2013 ).

Mshauri wa kisayansi katika mradi wa kitaifa wa kuandika mambo ya kale ya Misri ya kale mnamo kipindi cha (2005-2007).

Profesa katika Idara ya Mwongozo wa Kiutalii, Kitivo cha Utalii na Hoteli, Chuo Kikuu cha Helwan, tangu 2011.

Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu Huria kutoka (2010 – 2012).

Mkuu wa Idara ya Mwongozo wa Kiutalii, Kitivo cha Utalii na Hoteli, Chuo Kikuu cha Helwan, mnamo (2011-2012).

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya “Makumbusho ya Misri” huko Kairo, Helwan mnamo (2011-2012).

Mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Kifaransa ya Akiolojia ya Mashariki kutoka 2011-2015.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi IFAO huko Paris tangu 2011.

Mtaalamu wa kisayansi mshiriki katika Taasisi ya Ufaransa ya Akiolojia ya Mashariki huko Kairo kuanzia 2012-2015, na mtafiti mshiriki katika taasisi hiyo hiyo kuanzia 2002-2016.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Utalii na Hoteli za Elimu na Masuala ya Wanafunzi (2012-2013).

Mjumbe wa Delagation ya Misri katika kikao cha 18 cha Kamati kiutendaji ya Kampeni ya Kimataifa ya Uanzishaji wa Makumbusho ya Nubia.

Msimamizi mkuu wa mradi wa “Makumbusho ya Misri ya Ustaarabu wa Misri” kutoka (2014-2016).

Msimamizi mkuu wa “Makumbusho ya Misri” huko Tahrir kati ya 2015 na 2016.

Mwanachama wa misheni tatu za zamani za kiakiolojia za Ufaransa na Misri huko Atfih, Misri.

Mjumbe wa ujumbe rasmi wa Misri kwenye Mkutano wa 11 wa Kimataifa wa Wana-Egypt huko Florence, Italia.

Mjumbe wa ujumbe rasmi wa Misri kwenye Mkutano wa 9 wa Kimataifa wa Wanataalamu wa Misri huko Grenoble, Ufaransa.

Mjumbe wa kamati ya kisayansi ya “ENIM” – jarida la kwanza la Misri la Egyptology mtandaoni.

Mjumbe wa kamati ya kisayansi ya jarida la “Egypte” la Kifaransa.

Mwanachama sambamba wa Taasisi ya Akiolojia ya Ujerumani huko (Berlin) tangu 2015.

Mwanachama wa heshima wa Jumuiya ya Ufaransa ya Egyptology nchini Ufaransa tangu 2016.

Mwezi Machi mwaka wa 2016 , Dkt. Khaled al-Anani alishika wadhifa wa Wizara ya Mambo ya Kale ya Misri katika serikali ya Dkt. Sherif Ismail na kuendelea na Wizara katika serikali ya Dkt. Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, hadi Agizo lilipotolewa mnamo  Desemba 22, 2019 la kuchukua jukumu la Wizara ya Utalii baada ya kuiunganisha na Wizara ya Mambo ya Kale, na ndiye Waziri wa kwanza aliyeshikilia Wizara hizo mbili pamoja  tangu kutengana kwao mnamo 1966 , na Al- Anani aliendelea katika nafasi yake hadi mwaka 2022.

Dkt. Khaled Al-Anani ameshinda tuzo na nishani nyingi, zikiwemo:

Nishani ya Fares katika Sanaa  – Ufaransa (2015).

Nishani ya Kustahiki – Poland (2020).

Nishani ya Al-Shams Al-Moshreka – Japan (2021).

شاهد أيضاً
إغلاق
زر الذهاب إلى الأعلى