Vijana Na Michezo

DKT. MSONDE AKABIDHI BENDERA KWA TIMU YA TANZANIA INAYOSHIRIKI MASHINDANO YA FEASSSA NCHINI RWANDA

0:00

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amekabidhi bendera ya Tanzania kwa timu za Wanafunzi, Walimu na viongozi  wanaoenda kushiriki katika  Mashindano ya 21 ya michezo ya shule za Msingi na Sekondari ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSSA) yanayofanyika nchini Rwanda.

Makabidhiano hayo yamefanyika  leo Agosti 17, 2023 katika shule ya Sekondari Rusumo wilayani Ngara Mkoani Kagera wakati msafara wa timu hizo ukielekea nchini Rwanda.

Akizungumza na Wanafunzi, Walimu na Viongozi wanaoenda kushiriki Mashindano hayo, Dkt. Msonde amewata kila mmoja wao kujituma na kutumia umahiri wako kwa kila mchezo huku wakitambua kuwa wanaliwakilisha Taifa la Tanzania katika mashindano hayo.

Aidha, Dkt. Msonde amesisitiza upendo, umoja na mshikamano kwa washiriki wote ambao wataungana nao katika Mashindano ya FEASSA ambayo yatashirikisha nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rwanda, DR Congo, Kenya, Uganda.

Mashindano hayo yataanza tarehe 17-27 Agosti 2023 ambapo Tanzania itashiriki katika michezo ya Soka, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Hockey, Tennis, Riadha, Mpira wa Mikono na Netboli.

Back to top button