Chuo kikuu cha Al-Azhar ..Chuo kikuu kikubwa zaidi Duniani
Kimeanzishwa kabla ya Chuo kikuu cha Polonia huko Italia, pia kinazingatiwa chuo kikuu cha tatu cha zamani zaidi baada ya vyuo vikuu vya Al Zaitunah na um Al Qura, lakini wakati wote kimebaki taasisi ya kielimu wakati ambapo taasisi mbili zile zimeacha jukumu lao kama taasisi za kielimu, nayo ni Taasisi ya kidini, ya kielimu, ya kiislamu, ya kwanza na kubwa zaidi Duniani, na hupatikana mjini Kairo, Mji mkuu wa Jamhuri ya Misri ya kiarabu pamoja na matawi yake katika mikoa tofauti mengi ya kimisri .
Chuo kikuu cha Al Azhar ni mwelekeo wa waislamu wa kitaalam tangu zaidi ya miaka elfu moja ambapo ni mnara wa elimu na mwelekeo kwa wanafunzi wa kila mahali ili kujifunza elimu za kidini , kiarabu na sayansi ya asili na ya kibinadamu , na kinabaki katika historia ndefu yake kuwa kituo cha wepesi na msimamo wastani na kueneza utamaduni wa kiislamu , utaalam wa kiislamu na mafundisho ya uvumilivu vyake yasiyojua kutia chumvi au ukali , msimamo mkali au kushikia kibaya wa kimadhehebu na kisiasa … Na kwenye viwanja vyake wafalme , masultani , marais , masheikh wa Al-Azhar , mufiti, mawaziri , mabalozi , wataalam na wengineo kutoka maeneo ya ulimwenguni wamepata elimu.
Chuo kikuu na Msikiti :
Chuo kikuu cha Al-Azhar kilirithi Msikiti wa Al-Azhar unaorejea historia yake kwa zama ya Fatimi ambapo Ghawhar El-Sakaly aliweka jiwe la msingi kwa amri ya khalifa Al-muizz li din Allah El-fatmy mnamo Ramadhani 14 mwaka wa 359 AH (971AD) na Al-zahar iliteuliwa kama msikiti rasmi ambapo ulianzishwa na nchi kwa kuwa mnara wa uhubiri wa kidini na Alama ya utawala wake na msikiti huo ulifunguliwa kwa sala kwa mara ya kwanza mnamo Ramadhani 5 mwaka wa 361 AH na uliitwa kwa jina la Msikiti wa Al-Azhar kwa ajili ya bibi Fatma Al-zahra _ Mwenyezi Mungu amuwie radhi_ ambaye wafatmeen wanazingatiwa kuwa pamoja naye.
Na lengo la kuanzishwa kwake mwanzoni ni kuhubiri kwa madhehebu ya kishia na haikupitii muda mrefu ila ukawa chuo kikuu cha kueneza madhehebu ya kisunna ambapo wanafunzi hupokea taaluma mbalimbali za kidini na kimantiki na shukurani ya kupa Al-Azhar jukumu la kitaalam inarejea kwa waziri Yaqub bn Kals ambapo alimshauri khalifa El-azizz mnamo mwaka wa 378 AH kuubadilisha kwa chuo cha masomo baada ya vyuo kuwa kwa ibada ya kidini tu na kueneza madhehebu ya kishia .
Masomo yalianza kweli kwenye msikiti wa Al-Azhar mwishoni mwa enzi ya Al-muizz li din Allah Al-Fatmy wakati jaji Abu El hassan bin namaani Al-maghribi alipokaa mwaka wa 365 hijira ( Oktoba 965 BK ) katika kikao cha kwanza cha kitaalam kisha vikao vya kielimu viliendelea baada ya hapo .
Na vikao vya elimu vilikuwa msingi wa masomo katika Al-Azhar ( chuo kikuu na msikiti ) ambapo mwalimu anaketi ili kusoma somo lake mbele ya wanafunzi wake na wasikilizaji wanaomzungusha. Vilevile , wataalam wa dini wanaketi katika mahali wanapopewa kutoka maeneo yake . Na mwalimu haruhusiwi kufundisha ila baada ya kuruhusiwa na porofessa wake kulingana na mfumo wa mtihani wa mazungumzo katika mada kumi na moja na ruhusa ya kufundisha hutolewa na khalifa .
Al-Azhar ( Msikiti na chuo kikuu ) katika mfumo wake wa kielimu ni ya kwanza inayovumba mfumo wa mwanachuoni ulimwenguni kote na kazi ya mwalimu msaidizi huyu ni kurejea tena yale yaliyosemwa na mwalimu kwa mwanafunzi . Na inapaswa kwa mwanafunzi anayetaka kufundisha ni kupitisha mtihani na kabla ya hayo kupendekezwa na wataalamu wawili miongoni mwa wataalam wakubwa wa Al-Azhar tukufu . Ikiwa akipendezwa na akipata tazkia kutoka kwa wataalamu wawili atatoa ombi pamoja na wasifu wa sheikh wa Al-Azhar katika historia yake halafu sheikh wa Al-Azhar akaunda kamati ina wataalamu 6 wanaoongozwa na sheikh wa Al-Azhar na inaongezeshwa kwao mwanachama mwengine kama mwanafunzi anataka kufanya mtihani katika madhehebu ya El-Hanbaly na uamuzi wa kamati unatolewa na sheikh wa Al-Azhar ambapo kila madhehebu mmoja inawakilishwa na masheikh wawili , na mtihani huo ulikuwa ukifanyika midomoni na hauainishwi na wakati maalum , basi mwanafunzi anafanya mtihani katika mada kumi na moja siyo vitabu kumi na moja anavikumbuka vizuri midomoni , kama akieleweka vizuri ataruhusiwa kuwa mwalimu kuanzia muhadhara wa tatu yaani atakuwa mwalimu msaidizi kisha atapishwa baadye ili akawa mwalimu kuanzia muhadhara wa pili .
Chuo kikuu cha Al-Azhar kilitoa katika tarehe hiyo yale yanayoshindana na vyuo vikuu kutoka mfumo wa masaa ya elimu zaidi na kumpa masomo kwa zaidi ya mwalimu moja na mwanafunzi anaweza kuchagua na ilipatikana mhusika zaidi ya moja kwa kila mada na mwanafunzi ndiye anamchagua sheikh wake bila ya kumlazimisha kukaa hapa au pale … Hivi ndivyo mafunzo ya hiari yalikuwa huku kwenye chuo kikuu. Vilevile , mafunzo ya mtihani wa mazungumzo nayo ni mtihani bora zaidi .
Anayefikiri kwamba ukale wa chuo kikuu cha Al-Azhar haukurejei kwa mwaka 972 hijira na unarejea kwa mwaka 1920 anakosa kwa kiasi kikubwa, kwani uamuzi wa agizo la kifalme unakuja katika mfumo wa kihistoria wa kuendeleza elimu katika Al-Azhar ambayo ni jambo la kawaida kuiendeleza katika kila kipindi .
Wataalamu wa Al-Azhar wanafanya kazi zao za kufundisha vizuri na hawafundishi elimu ya kidini tu bali walifundisha falsafa , Mantiki , hisabati na matibabu japo kwa kiwango kidogo mwanzoni mpaka ElHakm b Amri allah alianzisha ” nyumba ya hekima ” na wanawake walihudhuria masomo kadhaa . Hivi karibuni masomo yalipanuka hadi yalijumuisha Elimu ya unajimu , Hesabu , Matibabu , ujenzi , kijiolojia , Historia na Elimu za kijamii kadhaa na elimu mbalimbali nyinginezo . Na kuhusu wataalamu mashuhuri ambao majina yao yaliambatana na Al-Azhar ( msikiti na chuo kikuu) ni :- Bn Khaldun , Ibn Taghri Bardi ,Musa Bin Maimon, Al Hassan Ibn Al Haytham , Muhammed Ibn Yunus Al Masry , Al Qalqashandi na wataalamu wengine walitoa matunda ya utaalam kwa duniani kote ambao umenufaisha utu hadi leo.
Ingawa kuwa hotuba ya Ijumaa ilisitishwa kufanyika kwenye msikiti wa Al-Azhar kwa takribani miaka mia moja wakati wa enzi ya kiayubia ila kuna ushahidi wa kuendelea masomo huku wakati mwingine . Shukrani ya kurudisha hotuba kwake chini madhehebu ya kisunna inarejea kwa sultani El Dhahir bebars Al-bandaqady ambapo aliujenga upya na kuurekebisha hapo hapo Al-Azhar ilirejesha nafasi yake kama kuwa ni chuo kikuu cha utaalamu ambacho kina uthamini mkubwa huko Misri na ulimwengu wa kiislamu .
Enzi ya Mamluki inazingatiwa kuwa mojawapo ya enzi zinazojipambanua kwa Al-Azhar (msikiti na chuo kikuu ) ambapo ilisifika ilichukua nafasi yake kama kituo cha elimu , na iliongezekwa kwa maktaba na vitabu vyenye thamani mpaka maktaba yake yakawa mojawapo ya maktaba kubwa zaidi katika mashariki na duniani kutokana na uthamini na vito inavyo na ujenzi wake unaendelea kufanywa na masultani na wamamluki mpaka ikawa shule kuu mjini Kairo , na chuo kikuu kikubwa cha kiislamu ambacho hakishindani na chuo kikuu kingine ulimwenguni kote mwa kiislamu .
Ingawa uzembe na uthabiti uliobandisha elimu na fanii nchini Misri chini ya utawala wa kiuthumani ila kwamba chuo kikuu kinaendelea kuwa mahali pa Amani , elimu na maarifa . Vilevile , Al-Azhar ( Msikiti na chuo kikuu ) ilisimama mbele ya mapinduzi katika kipindi cha kampeni ya kifaransa nchini Misri , ambapo iliuunga mkono raia ili kumchagua Muhammed Ali kuwa mfalme wa Misri . Katika miongo hii mirefu , chuo kikuu kilikuwa chanzo pekee cha kufundisha sayansi na kuhitimu wafanyakazi na walimu wa nchi katika ulimwengu wa kiislamu .
Na katika zama ya kisasa pamoja na maendeleo yaliyotolewa na Muhamed Ali kulikuwa wanafunzi na wanahitimu wa chuo kikuu hicho tu ili wawe kiini cha taasisi mbalimbali za elimu zilizoanzishwa ili ziwe vituo vya elimu kwa mtindo wa kisasa wa ulaya . Vilevile , kilikuwa kiini cha ujumbe wa kielimu kwa ulaya ili kusambaza maarifa ya kisasa .
Mwishoni mwa karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini , chuo kikuu cha Al-Azhar kilishuhudia mwanzo wa kurekebisha na kujenga upya lengo lake kukigeuza kwa taasisi yenye mfumo wa kielimu unatumia mtindo wa kisasa , Wataalamu kadhaa waliongeza urekebishaji huo na wa kwanza wao ni Muhammed Abdu ambapo alipounda baraza la usimamizi la kwanza kwa taasisi hiyo katika Rajab mnamo 6 , mwaka wa 1312 hijira hii ilifuatiwa na kutolewa kwa sheria namba 10 kwa mwaka 1911 ambayo ilipanga masomo na iliyafanya kuwa awamu , iliweka mfumo kwa wafanyakazi , masharti ya kukubali wanafunzi na mfumo wa mitihani na vyeti , pia alianzisha taasisi inaisimamia inayoitwa baraza kuu la Al-Azhar .
Kwa mwendelezo wa kukuza taasisi hii ya kifahari , sheria ya namba 49 kwa mwaka wa 1930 ilitolewa ambayo kulinagana nayo Vitivo vya vitatu vya Al-Azhar vilianzishwa , navyo ni Vitivo :- Misingi ya dini , sheria na lugha ya kiarabu , na sheria hiyo ilielezea uwezekano wa kupanua katika kuanzisha vyuo vikuu vingine .
Vilevile , sayansi zisizo kisheria ziliingizwa katika vyuo vya Al-Azhar kama :- Hesabu , sayansi na masomo ya kijamii ili kuwezesha wahitimu wanapoingia kwenye Vitivo vya Al-Azhar mbalimbali , kisha sheria ya namba 26 kwa mwaka wa 1936 ikafuata ambapo iliundwa upya nafasi ya nne nayo ni masomo ya juu na mwenendo huo ulifikia kilele kwa sheria iliitwa ” sheria ya maendeleo ” ilitolewa tarehe Julai 5, 1961 chini ya namba 103 kwa lengo la kuandaa tena Al-Azhar na kwa mujibu wa sheria hiyo , ilifanyika kazi ya chuo kikuu cha Al-Azhar kwenye uwanja wake ambacho kinajumuisha kwa mara ya kwanza Vitivo vya elimu kadhaa kama :- biashara , matibabu , uhandisi na ukulima. Vilevile , kilifunguliwa milango ya masomo kwa msichana mwislamu kws kujenga chuo cha wasichana kinachojumuisha sehemu za kusoma matibabu , biashara , sayansi na masomo ya kiarabu,kiislamu na masomo ya kibinadamu . Vyuo vya kisasa na kisayansi kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar vinajipambanua kuliko vitivo vingine kwa kutilia maanani kwake masomo ya kiislamu pamoja na masomo maalumu .
Mifumo ya elimu katika chuo kikuu ilipanuka na haikuishii kwenye mipaka ya mahali na wakati bali ilipelekea kwa upande mpya na kisasa na ujumbe wake hauishii kwa mawaidha , kuongeza na kufundisha tu bali uligusa pande mbali ili kiwe na uongozi katika utafiti , huduma ya umma ya kiislamu , kutetea masuala yake na kueneza kiislamu chenye msimamo wastani kwa lengo la kukabiliana na makundi ya ukatili na yenye misimamo mikali ulimwenguni kote .
Utoaji wake bado unaendelea na kwa wengi na unaendelea kwa ujumbe wake wa nje na wajumbe wa tamaduni zake wanaokwenda nchi mbalimbali za Afrika , Ulaya , Marekani Asia na bara la Australia baada ya kuweka wakati historia ndefu yake misingi ya mifumo na desturi za chuo kikuu zinazojulikana na kuzitekelezwa katika vyuo vikuu duniani .
Sifa za mhitimu wa Al-Azhar
Chuo kikuu cha Al-Azhar kinajivunia kwa vitivo vya Sayansi kama ujivuno wake kwa vyuo vya kidini kwani vina jukumu kubwa ambapo vinawafundisha wanafunzi sayansi ya ulimwengu pamoja na mafunzo ya dini ili wabebe ujumbe wa Al-Azhar kwa wanabiadamu pahali popote wanapokaa .
Ujivuno huo ulitegemea historia ndefu ambapo mwanasayansi wa macho anayejulikana ” Al-hassan bin Al- Haytham alisoma katika Al-Azhar , Muhammed bin Yunus El-masry aliyefariki dunia mwaka 1009 mvumbuzi wa trigonometry ” Hesabu pia alisoma katika Al-Azhar . Vilevile , Al-Azhar ilikuwa imepokea wataalamu wasio waislamu Ili kufundisha huku kama msomi maarufu wa kiyahudi ” Musa Bin Maimon” ambaye aliishi huko nchini Andalusia .
Kwa hivyo kufundisha sayansi za vitendo na majaribio zilianza katika Al-zahar mnamo tarehe ile ile ya kufundisha sayansi za kiarabu na kidini pamoja na makundi ya wahitimu wa kwanza yalikuwa huko Abu Zaabal na idadi yao ilikuwa wanafunzi mia moja wote ni wanafunzi wa Al-Azhar ambapo matibabu nchini Misri ilijulikana kupitia wanafunzi wa Al-Azhar .
Na wakati huo Muhammed Ali Pasha alipotaka kutuma ujumbe wa elimu ili kuimarisha Misri , hakukuta yoyote isipokuwa taasisi ya Al-Azhar kwa hivyo jumbe tisa za elimu zilitoka kukwenda Italia , Ufaransa , Australia , Uingereza , Urusi na nyinginezo , na zaidi ya 70% ya wanachama wa ujumbe walikuwa Wanafunzi wa Al Azhar .. hawa ambao waliorudi Misri na walianzisha shule ya Al-Alsun ambayo ilikuwa baada ya hivyo chuo cha Al-Alsun .
Vilevile, walianzisha harakati za tarjama na shule ya kiufundi ya kijeshi na nyinginezo .
Na aliyewapendekeza wale ni Sheikh Hassan Al-Attar aliyeandika juu ya unajimu , hesabu na Jiografia na alikuwa sheikh wa Al-Azhar , na sheikh Al-damanhory aliyetunga zaidi ya vitabu 6 katika matibabu na elimu ya anatomia pia alikuwa sheikh wa Al-Azhar na alikuwa akiandika juu ya misingi ya sheria kama alivyoandika juu ya anatomia .
Kwa hivyo chuo kikuu kikuu cha Al-Azhar kilikuwa kimebeba njia za kuangaza na viongozi wa maendeleo ya nchi ya Misri ya kisasa kwani ndicho kama kiongozi wa kuelimisha kila mahali ulimwenguni mwa kiislamu na kila wakati kwa kiwango kinachopita kiasi wakati wake daima
Na mnamo kipindi chake chote , wahitimu wake walikuwa kutoka vijiji vya Misri na ulimwengu na katika miji ya Misri na ulimwengu pia , watu wa matabaka na mahali mbalimbali wanawaelekea kwake ili kutunzwa na kufaidiwa kwa utaalam wao.
Nafasi zinazopatikana na uwezo wa ushindani kwa chuo kikuu cha Al-Azhar
Na wakati wa kuzungumzia nafasi zinazopatikana na uwezo wa ushindani kwa chuo kikuu cha Al-Azhar ndiyo pekee nayo ni nafasi ya kisasa kwa chuo kikuu cha Al-Azhar tu kwani Al-Azhar kinahitajikwa wala hakihitaji na kwa uchache utakuta taasisi inayohitajikwa wala haihitaji lolote .. na chuo kikuu cha Al-Azhar kinajipambanua kuliko taasisi yengine duniani kwamba ndicho kinajumuisha wanafunzi wageni kutoka nchi 107 , na haipatikani taasisi ya elimu duniani inakusanya jinsia na rangi mbalimbali hizo kutoka nchi hizo isipokuwa chuo kikuu cha Al-Azhar na ukaribisho wake kwa wageni kwa gharama ya Al-Azhar umezidi zaidi ya miaka mia tano na hiyo miongoni mwao fursa zinazopatikana .
Vilevile , wahitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar wanahitajika kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni na hiyo miongoni mwa uwezo wa ushindani .
Idadi ya walimu wote kwenye chuo kikuu cha Al-Azhar inafikia walimu 15155 na wafanyakazi wa idara kwenye chuo kikuu ni wafanyakazi 13074 , hawa wote wanahudumia takribani wanafunzi wa kiume na wa kike 500000 na miongoni mwao wanafunzi wageni .
Katika chuo kikuu kuna vitivo vya vitendo 23 miongoni mwao vitivo vya kurudia na hilo linakisukuma kutoka mashindano kwa uongozi na kutofautisha na vyengine .ikiwa kwa mfano chuo kikuu chochote kina kitivo cha matibabu kimoja wakati huo huo chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo vya matibabu 40 . Na ikiwa chuo kikuu chochote kina kitivo cha sayansi kimoja , chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo vya sayansi 30. Na ikiwa chuo kikuu chochote kina kitivo cha uhandisi kimoja , basi chuo kikuu cha Al-Azhar kinajumuisha vitivo vya uhandisi 3 , Ama chuo kikuu chochote kinajumuisha kitivo cha ufamasia kimoja , chuo kikuu cha Al-Azhar kinajumuisha vitivo 3 vya ufamasia na kuna kimoja chini ya ujenzi huku Luxor , na ikiwa chuo kikuu chochote kina matibabu ya meno kimoja basi chuo kikuu cha Al-Azhar kina vitivo 3 vya matibabu ya meno na kuna kimoja kinajengwa sasa huku Luxor. Hayo yote yanaonesha uwezo wa ushindani wa chuo kikuu cha Al-Azhar hata katika upande wa vitivo vya vitendo.
Na ikiwa vyuo vikuu vingine vina hospitali moja basi chuo kikuu cha Al-Azhar kina hospitali 6 na kinatoa huduma ya matibabu kwa hadhira mara sita dufu inavyotolewa na chuo kikuu kingine .
Hayo yote yanaweka uwezo wa ushindani mbeleni kwani kina kisichopatikana katika chuo kingine bali kina hospitali ilifunguliwa hivi karibuni upana wake mita za mraba 124000 nayo ni hospitali kubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya kati na ndani yake uwanja wa ndege .
Mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar na sifa za wahitimu
Sifa za mhitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar zinazomfanya ashindane na mhitimu yeyote wa vyuo vikuu vya ulimwengu kwa sababu mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar inategemea misingi mitatu haipatikani katika taasisi ya utaalam mwengine ulimwenguni kote :
Kwanza :-
Chuo kikuu kinawafundisha wanafunzi wake elimu zinazonunuliwa yaani Quran tukufu na sunna .
Pili :-
Kinawafundisha elimu zinazotumika akili kama sayansi za machine zinazomfundisha mwanafunzi kuelewa vizuri kutokana na hayo mwanafunzi wa Al-Azhar. Anaelewa matini kwa maana kadhaa si maana moja . Ama anayesoma elimu zinazonunuliwa tu hatumii isipokuwa maana moja tu ili kutomkosea mwengine au kumkafirisha mtu kutoka dini na hayo hayapatikani katika Al-Azhar tukufu .
Tatu:-
Chuo kikuu kinawafundisha wanafunzi wake sayansi za vitendo- pamoja na elimu za kisheria na kiarabu – kwa hivyo mwanafunzi anakua mwenye busara ambapo akili haigombani na kunukuu na dini haigombani na dunia kutokana na hayo ikapatikana utofauti wa madhehebu .. na kumkubali fikra za mtu mwengine nchini Misri .
Kwa hivyo tunaona kwamba misimamo tofauti na kukubali fikra za mtu mwengine ni miongoni mwa sifa za Mtaala wa Al-Azhar ambapo tunaona katika nyumba moja mtu anayemwabudu Mwenyezi Mungu kwa madhehebu ya El-hanafy na mwengine kwa madhehebu ya El-shafy na wa tatu kwa madhehebu ya El-malaky bila mtu yeyote kumkasirisha mwengine au kumkosea .
Njia hii ya kufundisha kupitia elimu zinazonunuliwa , sayansi zinazotumika akili na sayansi ya dunia inaiunda akili inaweka kuelewa vizuri na inaweza kusambamba na maendeleo kutokana na hayo wahitimu wa chuo kikuu cha Al-Azhar wanafundishwa ujumuishaji katika sheria ya matini na kufundishwa kwamba sayansi zinazotumika akili ni chombo kinachowezesha kufahamu vizuri matini zinazonunuliwa .
Mwanafunzi anasoma Mtaala mpya katika vitivo vya kisheria nao ni :- “masuala ya kisasa ” unaogusa masuala mapya yote na utafiti wa kisayansi unaoandikwa katika chuo kikuu ambao unajadili masuala haya .. pia tulikua kujua katika Al-Azhar kwamba kisheria inaandikwa katika kila kipindi na inapaswa kuandika katika kila kipindi , sheria inakifaa . Vilevile , chuo kikuu kinaamini kwamba matini ni maalum na matukio hayana kikomo yaani lazima matini ziguse masuala na matukio mapya yote .
Kwa hivyo chuo kikuu kinaendelea kuwalea wana wake juu ya Mtaala wa busara na inasimamia zaidi ya miaka elfu moja .. na ulimwengu mzima ulikipokea kwa ukaribisho kwa hivyo mitaala ya chuo kikuu cha Al-Azhar inabaki kuwa urithi wa kweli kutoka urithi wa Mtume S.w na kupitia mitaala hiyo , ulimwengu ulielewa uthamini wa njia ya kiislamu “ujumbe na mtume ” kwa mtindo wa mitaala hiyo, wana wa dunia walitambua historia ya umma yetu , ustaarabu wake na wanaume na mashujaa wake walioifanya maendeleo . Vilevile, Imechukuliwa vigezo vya kweli kutoka elimu za Al-Azhar na chuo kikuu chake ambavyo watu wanapima vitendo vya maisha kupitia kwake na wanaelewa kipimo cha mema na mabaya sio katika upande wa mwenendo wa mtu tu bali kipimo cha mema na mabaya ya ustaarabu , tamaduni kwa mataifa , watu na jamii za wanadamu .
Chuo kikuu cha Al-Azhar kinabaki kuwa chanzo cha kisayansi na kielimu kwa waislamu na wengine kwa linaliambatana na elimu za kiislamu , lugha ya kiarabu na nyingine za kijamii na kibinadamu , na ambacho kiliweza kupitia hisa yake ya kisayansi , kielimu na kitamaduni pamoja na hisa yake kutoka utafiti wa elimu kutoa masuluhisho bora kwa matatizo yanayotishia jamii za kibinadamu katika nyanja zote tofauti.