Siasa

Balozi wa Misri mjini Juba akutana na Waziri mpya wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Sudan Kusini

Mheshimiwa Balozi Moataz Mustafa Abd El-Qader , Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri nchini Jamhuri ya Sudan Kusini amekutana na Bw. Pal My Ding, Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini humo , ambapo Balozi huyo alisistizia maagizo ya Uongozi wa Kisiasa wa Serikali ya Misri kwa kutolewa aina zote za msaada nchini Sudan Kusini Kwa ajili ya kufikia Amani , Utulivu na maendeleo ya kiuchumi, pia Balozi huyo alionesha maendeleo yote ya mahusiano ya pande mbili kati ya nchi hizo mbili katika nyanja tofauti na sekta za kiuchumi, zikiwemo Ushirikiano wa kipekee kati ya Wizara mbili za Maji na Umwagiliaji huko nchi hizo mbili na miradi ya kimisri nchini Sudan Kusini .
Kwa upande wake, Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini alielezea shukrani kwa juhudi kubwa zinazofanywa na Uongozi wa Kisiasa na Serikali nchini Misri kwa ajili ya kusaidia Serikali na Watu wa Sudan Kusini, akisifu miradi na programu za Ushirikiano zenye faida za kiuchumi na kijamii kwa maisha ya raia wa Sudan Kusini , vilevile, alisifu kiwango cha programu na miradi ya Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za umwagiliaji na usimamizi wa rasilimali za maji .
Back to top button