Habari Tofauti

Bandari ya Port Said ya kiutalii yajiandaa kupokea Meli ya Matumaini “Logos Hope”

Ali Mahmoud

Tarehe na Meli ya Matumaini inayotembelea Bandari ya Port Said kwa mara ya pili katika historia yake
Jumamosi, Desemba 31, 2022

Ofisi ya habari ya eneo la kiuchumi la Mfereji wa Suez lilitangaza kuwa bandari ya utalii ya Port Said inajiandaa kupokea Maktaba inayoelea “MV LOGOS HOPE” iliyokuja kutoka bandari ya Beirut na kwenye meli hiyo yalifanyika maonesho yaliyoelea ya vitabu katika ziara iliyo ziara ya pili baada ya kukomesha kwa zaidi ya miaka 12, na imepangwa kuwa meli kutia nanga kwenye “Bandari ya utalii ya Port Said” mnamo 4 Januari ijayo na itaendelea kwa muda wa siku 20; kuondoka katika tarehe 23 ya Mwezi huo huo, kabla ya kuendelea safari yake kwenda bandari ya Aqaba nchini Jordan.

Eneo la kiuchumi la Mfereji wa Suez linafanya maandalizi maalum ya kupokea tukio hili la kiutamaduni tangu siku chache, na pia limechukua hatua zote muhimu na mamlaka zote zinazohusika, kuongeza kiwango cha juu cha tahadhari kwenye bandari na maeneo yaliyoizunguka, kati ya uwepo mkubwa wa usalama kwa ajili ya usalama wa meli na kuwezesha harakati ya kushuka kwa abiria 350 kufanya safari za utalii za haraka kwa Kairo, linaloonesha uwezo wa eneo la kiuchumi kubeba meli za kiutalii kwa ukubwa wake na aina zake zote, kuwaweka salama na kutoa huduma zinazohitajika kwao, ambalo husaidia kuvutia meli zaidi kwenye bandari za Misri.

Imepangwa kwa Meli kufungua maonesho yake yanayoelea kwa maelfu ya wageni kila siku kutoka kwa wanafunzi na wapenda-kusoma katika vikundi vya umri kati ya miaka 13 na 65, kwa malipo kidogo tu ya kutembelea meli hiyo na kushiriki katika shughuli zake, wakati watoto chini ya umri wa miaka 13, na Qaderoon Bikhtilaf wanaweza kuingia meli kwa bure, kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nne jioni kila siku kwa muda wote wa maonesho, kuanzia saa tisa Ijumaa jioni, na maonesho itafungwa siku ya Jumapili.

Inatajwa kwamba meli ambayo urefu wake unafikia mita 132 kwa muda mrefu inaainishwa kuwa maktaba kubwa zaidi Duniani iliyoelea, na idadi ya timu yake inafikia zaidi ya wajitolea 400, kutoka zaidi ya uraia 60 mbalimbali, na inamilikiwa na Shirika la Ujerumani la kufadhili “Vitabu vizuri kwa watu wote”, na maktaba yaliyoelea inajumuisha zaidi ya vichwa elfu 50, na inalenga, kwa utajiri wake wa kitamaduni, kueneza utamaduni duniani kote, na pia inaonesha katika eneo la mapokezi, filamu fupi inayoweka tarehe ya ziara za meli kwa bandari muhimu zaidi Duniani, na maonesho ya maingiliano kuhusu meli ya kisasa ya kuwajulisha umma kwake, meli hiyo imetembelea zaidi ya bandari 480 katika zaid nchi 150 na imepokea zaidi ya wageni milioni 49 ndani yake kupitia miaka 13, na bado huinua kauli mbiu wazi nayo ni “kubadilishana habari na kutoa msaada na matumaini” katika kila bandari inayoitembelea.

Back to top button