Habari

Balozi wa Misri mjini Conakry awasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Guinea

 

Rais wa Guinea, Luteni Jenerali Mamady Doumbouya, alipokea hati za Balozi Hassan Salah El-Nashar kuwa Balozi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri kwa Serikali ya Jamhuri ya Guinea. Baada ya sherehe za mapokezi, mkutano wa nchi mbili ulifanyika kati ya Rais wa Guinea na Balozi wa Misri, kwa mahudhurio ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri, Mkurugenzi wa Ofisi ya Rais na Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea, ambapo mkutano huo ulijadili mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili na njia za kuziimarisha kuelekea upeo mpya, ikiwa ni pamoja na maeneo yaliyopo ya ushirikiano na njia za kuziendeleza.

Rais wa Guinea alianza mkutano huo kwa kuomba kufikisha salamu zake kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, akielezea kufurahishwa kwake na mambo mbalimbali ya msaada wa Misri kwa Guinea, haswa programu za mafunzo zinazotolewa na Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Misri, linalochangia kwa kiasi kikubwa kuongeza ufanisi wa makada wa Guinea katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande wake, Balozi wa Misri alifikisha salamu za Rais Abdel Fattah El-Sisi kwa Rais wa Guinea, na akasisitiza kina na nguvu ya mahusiano ya kihistoria na kisiasa kati ya nchi hizo mbili, akielezea nia yake ya kufanya kazi ili kuziboresha pamoja na kusukuma kasi ya mahusiano ya kiuchumi na kibiashara ili kufikia matarajio ya nchi hizo mbili. Pamoja na kuendelea kwa uratibu na muunganiko wa maoni kati ya nchi hizo mbili kuhusu masuala mengi ya kikanda na kimataifa ya maslahi ya pamoja.

Back to top button