LAAC yataka ukamilishwaji soko la Tarime

Kamati ya Kudumu ya Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC) imeielekeza Halmashauri ya Mji wa Tarime kuhakikisha ujenzi wa soko unakamilika kwa wakati ili lianze kutoa huduma kwa wananchi na halmashauri ikusanye mapato.
Maelekezo hayo yametolewa leo Machi 22, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Staslaus Mabula mara baada ya kukagua ujenzi wa soko pamoja na jengo la Utawala la halmashauri hiyo.
Amesema kwa mujibu wa mkataba, tayari mkandarasi ameshaomba kuongezewa zaidi ya mara nne ili aweze kukamilisha soko ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
“Mkurugenzi huu ni muda wa mwisho, Kamati inagiza hadi kufikia tarehr 17 Mei mwaka huu soko liwe limekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.”
Kamati imeielekeza Halmashauri ya Mji wa Tarime kuhakikisha inafuata taratibu na miongozo kila wanapoanza kutekeleza miradi mbalimbali ili upunguza hoja za wakaguzi
Kuhusu ujenzi wa jengo la Utawala, Kamati imeridhika na utekelezaji wa mradi huo na kusema kuwa jengo limejengwa kwa ustadi na ubora unaohitajika
“Ipo tofauti kubwa kati ya jengo la Halmashauri ya Mji wa Tarime na majengo mengine, jengo hili limenengwa kwa ustadi mkubwa na viwango vya hali ya juu,hii ndivyo inavyotakiwa kwani thamani ya fedha zilizotolewa inaakisi ubora wa majengo,” amesema mheshimiwa Mabula
Adha, Kamati ya LAAC imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa matumizi mazuri ya fedha ambapo ameweza kununua samani za ofisi, ujenzi wa uzio pamoja na kibanda cha mlinzi kwenye fedha za ujenzi wa jengo la Utawala shilingi bilioni 2.9