Habari Tofauti

ZANZIBAR KUWA NA VITUO VYA KISASA VYA MABASI

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema ni wakati sasa Zanzibar kuwa na miundombinu bora  kwa kutenga maeneo maalumu kwa kujenga vituo vya kisasa vya mabasi ya kuondokea na kufikia pamoja na maegesho ya magari.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo leo  wakati wa Hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Mradi wa Kituo cha  kisasa wa Mabasi Kijangwani kinachojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 31 Disemba 2023  katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Kituo hicho cha kisasa cha Mabasi kitakuwa na Majengo mawili ya biashara ya ghorofa moja ikiwemo maduka ya kisasa, maegesho ya magari , maeneo ya ibada, na huduma mbalimbali za jamii.

Back to top button