Habari Tofauti

Dkt. Jafo asema mwitikio wa uwekezaji wa Biashara ya Kaboni umezidi kuongezeka kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyofanywa na Serikali.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) amesema mwitikio wa uwekezaji wa Biashara ya Kaboni umezidi kuongezeka kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyofanywa na Serikali.

Amesema hadi sasa kampuni 34 tayari zimesajiliwa na kuwa milango ya uwekezaji wa biashara hiyo ipo wazi huku akisisitiza Serikali inaendelea kuwakaribisha na kuwaunga mkono wawekezaji wote.

Dkt. Jafo amesema hayo alipokutana na kuzungumza na wadau wa Biashara ya Kaboni jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa wakati Tanzania inapokwenda kushiriki Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) itatumia fursa hiyo kuieleza dunia kushu fursa hiyo.

Aidha, Waziri Jafo amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ufuatiliaji Kaboni (NCMC) Prof. Eliakimu Zahabu kuhakikisha wanatatua haraka changamoto zinazojitokeza katika usajili wa biashara hiyo.

Amesema ni vyema kuona vijana wakinufaika na biashara ya kaboni kwa kupata na wakati huo Serikali ikipata mapato pamoja na mazingira kuwa salama zaidi kwa kuwa kila mtu atalinda cha kwake.

“Serikali ipo nanyi kuwasiiliza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan anawategemea sana katika ajenda yake hii ya biashara ya kaboni ndio maana mikutano yake yote anazungumzia biashara hii, hivyo tuisaidie nchi kwani utajiri tuliokuwa nao tukiutumia vizuri nchi yetu itakuwa ya mfano,” amesema Dkt. Jafo.

Kwa upande wake Prof. Zahabu amesema kituo hicho kimekuwa na uwazi na wakati huo kipo kuwezesha mchakato kwa kila mtu anayehitaji kufanya usajili au huduma yoyote kuhusiana na kaboni.

Back to top button