Kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi mbili za kidiplomasia za Misri na Sudan Kusini

Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia ya Wizara ya Mambo ya Nje iliandaa ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Sudan Kusini, ukiongozwa na Naibu Balozi Mayan Doot Well, kujadili njia za kuendeleza mambo ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Kidiplomasia ya Misri na Taasisi ya Diplomasia ya Sudan Kusini katika uwanja wa mafunzo na kubadilishana kidiplomasia.
Wakati wa ziara ya Katibu Mkuu na ujumbe wake ulioambatana, mkataba wa makubaliano ulisainiwa ili kuimarisha na kupanua mifumo ya mahusiano ya ushirikiano kati ya taasisi mbili za kidiplomasia, kulingana na mahusiano ya kirafiki kati ya Misri na Jamhuri ya Sudan Kusini katika ngazi ya nchi mbili.
Mkataba huo wa makubaliano ulisainiwa kwa niaba ya Misri na Balozi Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa upande wa Sudan Kusini, kwa mahudhurio ya Balozi Hossam Issa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan na Sudan Kusini, Balozi Walid Haggag, Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kidiplomasia, Balozi wa Sudan Kusini mjini Kairo, wajumbe wa Menejimenti ya Taasisi hiyo na ujumbe ulioambatana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini.
Wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo, Balozi Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika, alielezea fahari ya Misri katika mahusiano ya ushirikiano kati ya Misri na Sudan Kusini katika ngazi mbalimbali na ahadi ya Misri ya kuendelea kuendeleza mahusiano haya katika nyanja mbalimbali ili kutumikia malengo na maslahi ya nchi hizo mbili na watu wake, ikiwa ni pamoja na kusaidia upande wa Sudan Kusini katika kuendeleza Taasisi ya Kidiplomasia na kujenga uwezo wa makada mbalimbali katika vyombo vya dola nchini Sudan Kusini.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje wa Sudan Kusini alisisitiza shukrani zao kubwa kwa mahusiano ya kindugu ulio na mizizi kati ya nchi hizo mbili na nia ya Misri ya kusimama na Sudan Kusini na kuipatia msaada wote unaohitaji, akibainisha haswa hamu yao ya kufaidika na utaalamu wa kidiplomasia wa Misri katika uwanja wa mafunzo ya kidiplomasia na kufuzu kwa makada wao wa kidiplomasia na serikali, na kuongeza ushirikiano na kubadilishana kati ya taasisi za kidiplomasia za Misri na Sudan Kusini kwa mujibu wa mkataba mpya wa maelewano uliohitimishwa kati ya pande hizo mbili.