Habari
RAIS DK.MWINYI AWASILI DODOMA KUHUDHURIA KIKAO CHA NEC

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasili Jijini Dodoma kuhudhuria kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).
Katika uwanja wa ndege wa Dodoma amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule na viongozi wengine wa Mkoa huo.










