RAIS SAMIA:SERIKALI IMEWAPUNGUZIA MZIGO WA KUSOMESHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema serikali imewapunguzia wazazi gharama za kuwasomesha watoto kwa kujenga shule na kuondoa ada.
Dkt.Samia ameyasema hayo Oktoba 18, 2023 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Puge akiwa njiani kuelekea Tabora.
Amesema serikali imejenga shule kuanzia awali hadi sekondari bila kuchangisha hata shilingi na pia imeondoa ada hivyo wazazi wanawajibika kwa kununua sare na vifaa vya shule.
“Isingekuwa miradi hii ya Elimu wazazi mngetoa fedha nyingi sana kujenga shule lakini pia kulipa ada ya mtoto, hii ina maana kwamba Serikali imekuachia kipato chako ubaki nacho mfukoni, Serikali Ile gharama inabeba yenyewe ni kama Serikali inalipa mshahara kwa kila mzazi,”amesema