MAMA MARIAM MWINYI AKUTANA NA KATIBU MKUU UWT TAIFA JOKATE MWEGELO
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jokate Mwegelo na ujumbe wake Ikulu Migombani leo tarehe 17 Oktoba, 2023.
Mama Mariam Mwinyi amempongeza Jokate kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa UWT na kumueleza kuwa ni msichana machachari , mwenye akili ataweza kuisadia Jumuiya hiyo kwa mawazo mapya tofauti.
Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa lengo kubwa la Taasisi ya ZMBF ni kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuwaletea maendeleo ya kiuchumi Wanawake, Vijana na Watoto.
Jukumu nyingine la ZMBF ni kuwawezesha Wanawake na vijana katika kilimo cha Mwani zao ambalo ni la tatu kwa kuiletea Zanzibar fedha za kigeni .
Pia wamezungumzia suala la udhalilishaji wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto pamoja na Afya ya lishe.
Mama Mariam Mwinyi ameishukuru UWT kwa wazo la kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kutimiza miaka mitatu shamrashamra zitazofanyika tarehe 04 Novemba 2023 viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Naye, Katibu Mkuu wa UWT Jokate Mwegelo amesema UWT itabeba agenda zote za kuwasema na kuwatetea Wanawake nchini.
Amepongeza mabadiliko ya maendeleo yanayofanywa Zanzibar chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nane ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi .
Vilevile ameipongeza Taasisi ya ZMBF kwa kuwafikia wananchi katika kampeni ya Mariam Mwinyi Walkathon ambayo imewagusa na kuwafuata walipo kwa kupata uchunguzi na matibabu ya afya zao.
Katibu Mkuu Jokate Mwegelo aliwasili jana Zanzibar baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa hivi karibuni.