Habari
MAMA MARIAM MWINYI ASHIRIKI DHIFA BURUNDI
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi ameshiriki katika dhifa ya taifa iliyoandaliwa na Mke wa Rais wa Burundi Mhe. Mama Angeline Ndayishimiye Hoteli ya Kiriri Bujumbura, Burundi tarehe 08 Oktoba 2023.
Hafla hiyo ya chakula cha usiku imehudhuriwa pia na Mke wa Rais wa Kenya Mhe. Mama Rachel Ruto .
Mama Mariam Mwinyi katika hafla hiyo alikabidhiwa zawadi maalum na Mke wa Rais wa Burundi Angeline Ndayishimiye na baadae Mama Mariam akamkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Burundi na Mke wa Rais wa Kenya.