Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa yapitisha azimio la kukaribisha michango ya Jukwaa la Vijana Duniani huko Sharm El Sheikh
Tasneem Muhammad
Jumuiya Kuu ya Umoja wa Mataifa imepitisha azimio la mifano ya Umoja wa Mataifa na jukumu lao katika kuwawezesha vijana, kuimarisha mawasiliano yao na Umoja wa Mataifa na kuimarisha ujuzi wao wa hatua za kimataifa.
Rasimu ya azimio hilo ilidhaminiwa na kundi la mataifa, ikiwa ni pamoja na Misri, Ureno, Jamaica, Jamhuri ya Dominika na Laos. Azimio hilo lilikaribisha michango ya vikao vya vijana na mikutano, hasa Jukwaa la Vijana Duniani huko Sharm el-Sheikh katika matoleo yake manne, katika kuwawezesha vijana na kuwapa fursa ya kuendeleza uwezo wao.
Balozi Osama Abdel Khaleq, Mwakilishi wa Kudumu wa Misri katika Umoja wa Mataifa mjini New York, alisema kuwa kupitishwa kwa azimio hilo, na kuingizwa kwa zaidi ya nchi 115 kwenye orodha ya wadhamini, kunaonesha shukrani ya kimataifa inayofurahiwa na Jukwaa la Vijana Duniani na inawakilisha jukwaa muhimu la kubadilishana mawazo na maono kati ya vijana wa kimataifa, haswa katika nyanja za amani, ubunifu na maendeleo, akisisitiza umakini wa uongozi wa kisiasa wa Misri kushinikiza na kuwawezesha vijana na kuongeza fursa zao za kushiriki katika juhudi zote za maendeleo. Balozi Abdel Khaled pia alisisitiza kuwa kupitishwa kwa azimio hili kunakuja kama muendelezo wa jukumu la Misri katika faili ya uwezeshaji wa vijana katika Umoja wa Mataifa, hasa baada ya kupitishwa kwa uamuzi wa kuanzisha Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Vijana mnamo Septemba 2022, Misri na Guyana zilizowezesha mashauriano ya serikali.