Habari Tofauti

MAMA MARIAM MWINYI AGAWA VIFAA VYA MWANI ZANZIBAR

0:00

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi  amesema zao la Mwani ni zao linaloelekea kushika kasi kubwa katika soko la Dunia wakati Zanzibar inashika nafasi ya kwanza katika kuzalisha zao hilo.

Ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya ugawaji wa vifaa bora vya kuanikia Mwani ambavyo ni vichanja vya kisasa 220 vyenye thamani ya zaidi ya milioni 289 kwa wakulima iliyofanyika Bweleo , Wilaya ya Magharibi B  Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Mama Mariam Mwinyi amesema zao  la Mwani ni dhahabu ya Zanzibar kwani unaleta tija ya kiuchumi na pia kwa mwili wa binadamu kwani Mwani ni chakula na una virutubisho vingi sana ikiwemo madini ya chuma ambayo yanaweza kutumika na kina mama wajawazito, Mwani pia hutumika kama mbolea kwa mazao mengine na vipodozi.

Vilevile, amesema ukiachana na Bara  la Asia ambao wanaongoza kidunia.Zanzibar inashika hatamu kwa kulima Mwani Afrika.

ZMBF imekuwa mstari wa mbele kukuza zao la Mwani kupitia lengo lake la kimkakati namba moja la kuwawezesha Wanawake na Vijana kiuchumi kupitia ukulima wa Mwani.

Amewashukuru Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa kushirikiana katika upatikanaji wa vifaa bora vya

Back to top button