RAIS DK.MWINYI ATOA WITO WA KUENDELEA KUIMARISHA NA KUVILINDA VYANZO VYA MAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya maji kwa kutekeleza miradi mikubwa katika sekta hiyo kama ilivyopangwa na kuelekezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050, ahadi alizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu pamoja na mipango mbalimbali ya maendeleo iliyopangwa na Jumuiya za kikanda na Kimataifa.
Ameyasema hayo leo akifungua Kongamano la Maji Zanzibar linalofanyika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Vilevile, Rais Dk.Mwinyi ametoa wito wa kuvisimamia vyanzo vya maji na kuhakikisha vinalindwa ili kuepusha uvamizi pamoja na kuandaa utaratibu wa utambuzi wa maeneo na kuyapatia hatimiliki kwa uendelevu wa vyanzo hivyo.