Habari Tofauti

Wastaafu wameshauriwa  kutumia  muda wao vizuri katika  kufanya  kazi ambazo zitawaingizia kipato ili kuepukana na umaskini

Rai hiyo imetolewa Agosti 11, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Njombe Ndugu Kuruthum Sadick katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Halmashauri ya Mji Njombe waliostaafu kuanzia Januari 2022 hadi December 2022.

Akitoa nasaha kwa watumishi thelathini na tano (35) waliostaafu, Mkurugenzi wa halmasahuri ya Mji Njombe aliwaomba wastaafu hao kutobweteka mara baada yakupata pensheni yao yakustaafu badala yake wajikite kweye shughuli za uzalishaji ili kujiongezea kipato.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe.Erasto Mpete amempongeza Mkurugenzi wa halmashauri mji Njombe kwa kuwa na utamaduni mzuri wa kuwaaga watumishi wanaostaafu kwa mujibu wa sheria

Amesema kitendo hicho kinaleta mshikamano na mahusiano mazuri katika jamii. Aidha amewaomba wastaafu hao kutumia uzoefu wao wa muda mrefu  kazini kutoa ushauri kwa watendaji walipo kazini pale wanapoona panahitaji ushauri .

Hafla hiyo ya kuwaaga wastafu ilifanyika katika ukumbi wa Johnson uliopo Njombe Mjini na ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Njombe,viongozi kutoka vyama vya wafanyakazi,Viongozi wa Dini pamoja na waheshimiwa Madiwani.

Back to top button