Habari

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA MSANII JIN DONG KUTOKA CHINA

0:00

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ujio wa msanii nyota maarufu wa filamu nchini China,  Jin Dong utaifungulia milango zaidi Zanzibar kwa soko la watalii kutoka China na kuitangaza kimataifa.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu, Zanzibar alipokutana na msanii huyo  ambaye yupo Zanzibar  kwa ajili ya  kutengeneza filamu.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi alimueleza msanii huyo kuwa Zanzibar ina vivutio vingi vya utalii ikiwemo utalii wa fukwe za bahari zenye mchanga mweupe zinazovutia wengi duniani, utalii wa utamaduni , utalii wa Mji Mkongwe,utalii wa michezo, utalii wa visiwa pamoja na wa Mikutano.

Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amemtembeza katika miongoni mwa vivutio msanii huyo ikiwemo kisiwa cha Mnemba, maeneo ya Mizingani, Forodhani pamoja  na Mji mkongwe .

Msanii Jin Dong  ni nyota mkubwa China mwenye  ushawishi na wafuasi katika mitandao ya kijamii zaidi ya Milioni 15 pia na kazi zake nyingi za filamu alizoigiza nchini humo .

Back to top button