Vijana Na Michezo

Ujumbe wa Morocco wafanya ziara huko Mji Mkuu Mpya wa Utawala

Zeinab Makaty

0:00

Wizara ya Vijana na Michezo ( Idara kuu ya maendeleo ya vijana), iliandaa ziara ya ujumbe wa Morocco kwa Mji Mkuu Mpya wa Utawala kupitia idara ya umma kwa Programu za kiutamaduni na za kujitolea, ndani ya matukio ya mpango wa kubadilishana ujumbe wa Misri na Morocco, kwa ushirikiano na idara ya umma wa mahusiano ya kimataifa, pamoja na uratibu na idara kuu kwa masuala ya Waziri, hivyo ndani ya mfumo wa kuendeleza na kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili kupitia vijana.

Shughuli za ziara hiyo ni pamoja na ziara ya ujumbe wa Morocco katika Kanisa Kuu jipya la Kuzaliwa kwa Kristo, kumbukumbu, pamoja na wajumbe wa ujumbe huo kutembelea wilaya ya serikali katika mji mkuu, na Jiji la Utamaduni wa Kiislamu.

Ziara hiyo ilihitimishwa kwa kutembelea kwenye mji wa michezo huko mji mkuu huo wa utawala, na kuona ukumbi wa ndani na viwanja vipya vya Olimpiki, wajumbe hawa wanaeleza furahi zao kubwa kwa walichokiona mjini mkuu kama maendeleo na ustawi yanayotolewa na nchi ya Misri.

Back to top button