Habari Tofauti

KITUO KIPYA CHA AFYA MAKOWO CHAANZA KUTOA HUDUMA

Kituo kipya cha afya Makowo kilichopo halmashauri ya mji wa Njombe kilichojengwa kwa zaidi ya shilingi milioni 600 kimeanza rasmi kutoa huduma mara baada ya kufungwa vifaa tiba ambapo watoto wawili wa kike wameweza kuzaliwa salama kituoni hapo na mmoja wa kwanza kupewa jina la Samia.

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe Isaya Mwasubila kwa niaba ya mkurugenzi amesema kituo hicho cha afya kimefungwa vifaa vya milioni 270 mpaka kuanza kwake kutoa huduma huku akiwashukuru wananchi kwa kuwa wavumilivu tangu kituo kilipoanza kujengwa mwaka 2017 kutokana na nguvu za wananchi pamoja na mapato ya ndani.

“Kabla ya yote nimdhukuru Rais Samia ambaye ametoa vifaa mpaka sasa vya shilingi milioni 120 kutoka serikali kuu lakini kupitia bajeti kuu ya 2022-2023 ilituwezesha halmashauri kutenga Milioni 150 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na kufanya jumla ya shilingi 270 ya vifaa vilivyofungwa na kuanza kutoa huduma hapa”amesema Mwasubila.

Kutokana na furaha walionayo wananchi kwa kituo hicho kuanza kutoa huduma na kusaidia wanawake wawili kujifungua watoto wa kike kwa mara ya kwanza,ndipo diwani wa kata ya Makowo Honolatus Mgaya (Luketulo) kwa niaba ya wananchi wakalazimika mtoto wa kwanza kumpa jina la Rais Samia  huku wa pili akipewa jina Iluminatha aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili kuenzi juhudi zao huku mbuge wa jimbo hilo Deo Mwanyika akitoa wito wananchi kutunza vifaa na kituo hicho ili kuendelea kuleta tija kwa wananchi.

“Kituo hiki kitahudumia watu wengi niombe vifaa vitunze na tumepamabana halmashauri tutapata magari mapya mawili na kwa mamlaka mliyonipa ninyi wananchi gari moja ni hapa Makowo”amesema Mwanyika

Yolanda Kipeta ni mama aliyeambatana kwa ajili ya kuwauguza wanawake waliojifungua katika kituo hicho ameshukuru madaktari kwa kufanikisha watoto kutoka salama huku Gelofravor Msemwa mwanamke mkazi wa kijiji hicho wakiishukuru serikali kwa kuwasaidia

Back to top button