Rais wa Kenya: Afrika ni bara la baadaye la nishati ya kijani na lachangia kutatua matatizo ya ulimwengu
Mervet Sakr
Rais William Ruto wa Jamhuri ya Kenya alisema, “Tumedhamiria kuliongoza bara la Afrika na kuungana pamoja ili kubuni suluhisho mwafaka na kuzitekeleza pamoja kwa ajili ya bara la Afrika.”
Rais wa Jamhuri ya Kenya aliendelea kusema: “Tumeungana pamoja ili kupiga hatua pamoja, akisisitiza kuwa bara la Afrika linachangia kutatua matatizo ya ulimwengu.
Rais huyo alisifu utendaji wa Rais Abdel Fattah El-Sisi wakati wa Uenyekiti wake wa NEPAD, uliopata mafanikio makubwa katika Ajenda ya Maendeleo ya 2063 na kumpongeza kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa hali ya hewa wa COP27 huko Sharm El-Sheikh.
Rais wa Jamhuri ya Kenya alisisitiza kuwa Afrika ni bara la baadaye la nishati ya kijani, akisisitiza kuwa Jumuiya za kiuchumi na mafanikio yao ni ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na bara la Afrika.
Hayo yamejiri wakati wa uzinduzi wa kikao cha 5 cha Mkutano wa Uratibu wa Mwaka wa Umoja wa Afrika, katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.