Ujumbe wa Misri washiriki katika mkutano wa 43 wa Baraza Kuu la Mawaziri wa Umoja wa Afrika
Mervet Sakr
Ujumbe wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri washiriki katika kazi ya kikao cha 43 cha Baraza Kuu la Mawaziri wa Umoja wa Afrika, kilichoanza leo na kitaendelea mnamo kipindi cha kuanzia Julai 13-14 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa uongozi wa Balozi Ashraf Sweilam, Waziri Msaidizi wa Mambo ya Nje na Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika na Mikusanyiko ya Afrika, na Balozi Dkt. Mohamed Gad, Balozi wa Misri nchini Ethiopia na Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika.
Baraza Kuu la Umoja wa Afrika linatarajiwa kuzingatia ripoti kadhaa juu ya masuala ya kifedha na kiutawala na bajeti ya Umoja wa Afrika kwa mwaka ujao, pamoja na ripoti kadhaa juu ya ufuatiliaji wa mchakato wa ushirikiano wa kikanda Barani na maendeleo yaliyopatikana katika mgawanyiko wa kazi kati ya Umoja wa Afrika na taratibu za kikanda na vikundi, pamoja na mchakato wa mageuzi ya kitaasisi ya Umoja wa Afrika, pamoja na kuzingatia masuala kadhaa ya kipaumbele, ambayo ni mabadiliko ya hali ya hewa na uanzishaji wa Mkataba wa Biashara Huria wa Bara.
Ikumbukwe kuwa Baraza Kuu linaloendelea linatangulia mkutano wa tano wa uratibu uliopangwa kufanyikwa Januari 16 jijini Nairobi.