Habari Tofauti

Siku ya Uhuru wa Algeria

0:00

Kumbukumbu ya miaka 61 ya Uhuru wa Algeria.. Mapambano ya nchi ya mashahidi milioni na kukumbatia Misri kwa mapinduzi ya Algeria

Leo, Watu ndugu wa Algeria  wanasherekea siku ya Uhuru ya miaka 61, Uhuru ambao ulilipwa na mashahidi zaidi ya milioni moja na nusu, ambapo Ukoloni wa kifaransa nchini humo uliendelea kwa miaka 133, unaondoa, unapora, unataka kufuta utambulisho wa Algeria na ulikomesha ukuaji wa kistaarabu wa nchi, na zima njia zote za upinzani wa watu wa Algeria na kuweka shinikizo kwao kwa njia za kikatili mbaya zaidi, Lakini mazoea ya ukoloni hayakufaulu katika kuzima upinzani na mapambano ya Watu wa Algeria na ujasiri wao katika kulinda ardhi yao, Upinzani wa wananchi ulijumuisha maeneo yote ya Algeria kwa ujumla, na mapambano yaliendelea hadi mapinduzi ya ukombozi wa Algeria yalipoanza mwaka 1954 kutangaza vita dhidi ya ukoloni na kukaribisha mwisho wake, Mapinduzi yaliendelea kwa miaka saba, na damu ya mashahidi ilimwagika kwa ajili ya uhuru hadi mapambano haya yalifikia kilele cha uhuru mnamo Julai 3, 1962.  Tarehe 5 Julai ilichaguliwa kusherehekea Siku ya Uhuru na Vijana pamoja.

Back to top button