DKT. MSONDE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA ELIMU URAMBO
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayesimamia Elimu, Dkt. Charles Msonde amewasili Wilaya ya Urambo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Sekta ya Elimu.
Leo tarehe 24 June 2023 amefanya ziara katika Wilaya Urambo na Kaliua na kukagua ujenzi wa Shule Mpya na Madarasa yanayoendelea kujengwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ujifunzaji katika Elimu ya Awali na Msingi (BOOST) pamoja na ujenzi wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano.
Aidha, Dkt. Msonde akiwa katika wilaya Urambo atakagua ujenzi wa Shule Mpya, Madarasa, Nyumba za Walimu na Vyoo katika Shule ya Jionee, Shule ya Urambo na Shule ya Sekondari Mapambano kwanza.