Rais Abdel Fattah El-Sisi Ijumaa Juni 23, mjini Paris alikutana na Bw. Bruno Le Maire, Waziri wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa.
Mshauri Ahmed Fahmy, Msemaji rasmi wa Urais wa Misri, alisema kuwa Rais alielezea nia yake ya kuimarisha na kuendeleza matarajio ya ushirikiano wa pamoja na Ufaransa katika nyanja za kiuchumi na maendeleo, haswa kupitia kuongeza uwekezaji wa Ufaransa nchini Misri kutumia fursa za kuahidi zinazotolewa na miradi mikubwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa alithibitisha nia ya nchi yake ya kuongeza ushirikiano na serikali ya Misri katika nyanja mbalimbali ambazo zitakuwa kwa maslahi ya mchakato wa maendeleo unaoendelea nchini Misri, akisisitiza msaada wa Ufaransa kwa miradi ya makampuni ya Ufaransa nchini Misri, na kutoa mifumo muhimu ya fedha kwa mipango ya nchi hizo mbili kwa mipango ya ushirikiano wa kifedha na kiufundi.
Tena Msemaji huyo aliongeza kuwa mkutano huo ulishughulikia shughuli za Kilele cha Mkataba wa Ufadhili mpya Duniani,na haja kubwa sana ya kufanya marekebisho mapya yenye manufaa katika shirika hilo la Ufadhili Duniani, kwa lengo la kuongeza Haki ndani yake na kukuza uwezo wa nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto zilizopo haswa suala la Mabadiliko ya hali ya hewa.