Uchumi

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais akutana na Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (OMR) , Bi. Mary Maganga, akiwa pamoja na Wataalam wa OMR akutana na Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia.

Ujumbe huo wa Benki ya Dunia umeongozwa na Bw. Nicholous Soikan – Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Mabadiliko ya Tabia Nchi – Benki ya Dunia.

Lengo la kikao hicho ni kujadili uandaaji wa Taarifa ya Kitaifa ya Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo (Country Climate Development Report).

Uandaaji wa taarifa hiyo utajikita katika kufanya tathmini ya uhusiano uliopo kati ya athari za Mabadiliko ya Tabianchi na ukuaji wa sekta za kiuchumi utakaowezesha nchi kupanga malengo ya maendeleo yanayazongatia hali halisi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.

Kikao hicho kimefanyika 22/06/2023,katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais mkoani Dodoma.

Back to top button