Habari

Kamati ya Kudumu ya Ufuatiliaji wa Mahusiano ya Misri na Afrika yafanya mkutano wake wa mara kwa mara katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje

Mervet Sakr

 Jumatano Juni 21, 2023, Kamati ya Kudumu ya Ufuatiliaji wa Mahusiano kati ya Misri na Afrika ilifanya mkutano wake wa kawaida pamoja na uenyekiti wa Balozi Hamdi Loza, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Mambo ya Afrika, kwa kushirikisha wawakilishi wa Wizara kadhaa na mashirika ya serikali yanayohusika.

Mkutano huo ulijadili njia za kuimarisha biashara kati ya Misri na nchi za Afrika, kufuatilia utekelezaji wa mpango mkakati wa kuongeza mauzo ya Misri kwenda Afrika ifikapo mwaka 2025, na hali ya miradi ya ushirikiano wa nchi mbili inayotekelezwa na Misri katika nchi kadhaa za bara hilo.

Back to top button