Dk.Hussein Ali Mwinyi atembelea Makumbusho ya Fuer Naturkunde
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ametembelea Makumbusho ya Fuer Naturkunde Jijini Berlin, Ujerumani tarehe 19 Juni 2023 .
Makumbusho haya yamehifadhi mabaki ya Dinosau ( Dinosaur) mkubwa aliyegunduliwa Tanzania Mwaka 1906/07 katika kijiji cha Tendaguru Lindi.
Masalia hayo yanakadiriwa kuwepo wakati wa Kipindi cha Jurassic cha mwisho takribani miaka milioni 150 iliyopita.
Pia ametembelea ukuta wa Berlin uliokuwa ukitenganisha Berlin ya Mashariki na Magharibu uliojengwa 13 Agosti 1961, ulidumu hadi 9 Novemba 1989. Ukuta huo ulijengwa na Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani (GDR) kwa lengo la kuzuia raia wa Mashariki ya Ujerumani kutoroka kwenda Magharibi.